RAIS SAMIA ASIKITISHWA KIFO CHA MKURUGENZI MTENDAJI TANESCO NA DEREVA WAKE - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Sunday, April 13, 2025

RAIS SAMIA ASIKITISHWA KIFO CHA MKURUGENZI MTENDAJI TANESCO NA DEREVA WAKE

 


RAIS Samia Suluhu Hassan kupitia taarifa yake, ambayo imepatikana amesema amesikitishwa na taarifa za kifo cha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mh. Boniface Gissima Nyamohanga na Dereva wake.

Kifo Mh. Nyamohanga na dereva wake  kimetokea leo mkoani Mara kwa ajali ya gari na kwa mujibu ya Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO itaendelea kutoa taarifa za utaratibu wa maziko.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya Mhandisi Boniface Gissima Nyamohanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), pamoja na dereva wake, Muhajiri Mohammed Haule, vilivyotokea usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya barabarani eneo la Bunda, Mkoa wa Mara.


Ninatoa pole kwa familia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko, watumishi wa TANESCO, ndugu jamaa na marafiki. 


Namuomba Mwenyezi Mungu azijaalie familia, ndugu, jamaa na marafiki subra, uvumilivu na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu," amesema Rais Samia.


Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. 


Amina.


No comments:

Post a Comment