SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUWEZESHAJI TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Monday, April 14, 2025

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUWEZESHAJI TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU


 NA MWANDISHI WETU


MAKAMU wa RAIS Dkt Philip Mpango, ametoa wito kwa Taasisi ya Elimu Tanzani  (TET) kuhakikisha tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Ubunifu zinakuwa endelevu na Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ya uwezeshaji.


Hayo yamebainishwa April 13, 2025 ikiwa ni Siku ya Kumbukizi ya Kuzaliwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambapo hufanyika hafla ya utoaji tuzo hizo na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega , akimwakilisha  Makamu wa Rais Philip Mpango katika shughuli ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam.


 Amesema tuzo hizo ni muhimu kwa kuwa zinaenzi Kwa vitendo yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa mtungi wa mshahiri na mtafsiri wa riwaya mbalimbali zilizokuwa Kwa lugha ya kingereza na kuziweka kwenye kiswahili, amesema.


Pia ameweka wazi kuwa tuzo hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza Kiswahili kutokana kwamba moja ya masharti ya utungi ni kutumia lugha ya kiswahili.


Aidha ameongeza kuwa Kwa sasa lugha ya Kiswahili inazidi kuvuka mipaka kwa mataifa mbalimbali kuingia mikataba na Tanzania kufundisha katika nchi zao.


Ameongeza kuwa kwa kazi ambazo zinapata nafasi ya miswada yao kuchapishwa inasaidia kuinua lugha ya kiswahili kutokana na kutumika kwenye shule mbalimbali nchini na kuwa sehemu ya dhana ya kufundishia.


Waziri Ulega kwa niaba ya Makamu wa Rais amewaasa was huu washindi wa nafasi ya nne hadi ya 10 ambao walitunukiwa vyeti vya ushiriki kutokata tamaa kwani bado wananafasi ya kufanya vizuri zaidi katika tuzo zijazo kwakuwa tayari wamepata uzoezi Kwa kutambua mashindano hayo yanataka vigezo gani ili ufanikiwa kushinda.


Naye Mhadhiri Mwandamizi, Mtungi na Mchoraji maarufu kutoka  Chuo Kikuu Cha Sultan Qaboos, Muscat nchini Oman, Prof. Ibrahim Noor Shariff, amefafanua kwamba kwa sasa Kiswahili kilipofika uwezi kumteta mtu kwani unaweza kudhani mtu akiliyekaribu yako hajui kiswahili kumbe la hasha na hapo ndipo unapoaibika.


(Pongezi kwa waandaaji wa tuzo hizo Kwani zinamchango mkubwa katika kukuza lugha ya Kiswahili na zinatengeneza vipajj vya watungi katika nyanja ya ushauri, riyaya nk,) amesema.


Pia alimuomba mgeni rasmi kufikisha salam zake Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuenzi Kiswahili kwa uwezeshaji wa tuzo hizo ambazo ni Tunu ya Taifa.


Pia Aneth Komba, Mkurugenzi Mkuu wa TET, amesema huu ni msimu wa tatu tangu tuzo hizo kuanzishwa na zimekuwa na mafanikio kwa watungi kuongezeka.



"Pia nimshukuru Rais Samia kwa jitihada zake katika kuwezesha tuzo hizo uendelea kufanyika ambazo zinatambua mchango wa Waandishi Bunifu," amesema.


Ameongeza kuwa mchakato wa tuzo zijazo zinaanza sasa baada ya msimu wa tatu kukamilika na watatoa utaratibu wakati wowote kuanzia sasa.


Penina Mrama, ambaye ni Mwenyekiti wa Jopo la  Majaji wa tuzo hizo, amesema kwamba ni jambo jema kuona aina za tuzo zinaongezeka ambapo awali zilikuwa mbili nazoi ni riwaya na ushairi na sasa zimefika nne zikiwemo hadithi zawatoto na tamthilia.

Washindi wa kwanza katika kila kipengere wamekabidhiwa mfano wa hundi ya  shilingi mil 10 kila mmoja na washindi wa pili katika kila kipengere amepatiwa mfano wa hundi ya sh. mil 7 na washindi watatu wamepatiwa mfano wa hundi ya sh. Mil 5 kila mmoja.






No comments:

Post a Comment