NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhinni (LATRA) imesema kuwa katika kipindi Cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuanzia Februari ,2021hadi Machi 2025 imetoa leseni 108,658 za usafirishaji sawa na ongezeko la asilimia 48.
Hayo yamebainishwa, Aprili 14,2025 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Suluo amesema katika kipindi cha miaka minne latra wameweza kufanikiwa kuongeza ofisi 10 katika Halmashauri za miji na wilaya na wanatarajia kuongeza ofisi nyingineV Tano hivi karibuni.
Pia wameweza kuongeza ruti 1007 kutoka Mbezi Luis hadi Kisarawe ili kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi.
Hata hivyo LATRA wameweza kuwathibitisha madereva 4563 kati ya madereva 9191 waliojitokeza kufanya mitihani ambapo madereva 4,563 wamepatiwa vyeti lengo la kufanya hivi ni kuboresha huduma na kupata madereva wenye weledi wa kuendesha magari yanayotoa huduma za usafiri wa umma na mizigo kwa usalama.
Jumla ya mabasi 2323 yanafanya safari za usiku ambapo zilianza Oktoba 2023 hii imetokana na usikivu wa Serikali ya awamu ya sita imepelekea kuwa na usafiri wa saa 24.Tangu kuanza Kwa safari Latra imeendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuratibu .
CPA Suluo amesema kwamba ,Utoaji Leseni kwa Vyombo vya Usafiri kwa Njia ya Barabara
Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1)( b) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, Sura ya 413, LATRA ina wajibu wa kutoa, kuhuisha, kusitisha na/au kufuta leseni za usafirishaji. Idadi ya leseni za usafirishaji zilizotolewa kwa vyombo vya usafiri wa abiria (passenger service vehicles), mizigo (goods carrying vehicles), na vyombo vya usafiri wa kukodi (private hire service vehicles) ziliongezeka kutoka 226,201 mwaka
Serikali ya Awamu ya Sita iliondoa zuio la mabasi ya abiria kusafiri nyakati za usiku
lililowekwa mwaka 1994. Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti
tarehe 28 Juni, 2023, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliziagiza, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Uchukuzi kuweka utaratibu mzuri wa usimamizi wa mabasi nyakati za usiku
LATRA ilishiriki katika zoezi la kufanya maandalizi ya kuanza kwa safari za
usiku kwa kushirikiana na wadau wake muhimu, hasa wamiliki wa mabasi (wakiwemo TABOA) na ilitekeleza maamuzi ya Serikali kwa kuanza kutoa ratiba za mabasi kusafiri usiku na mchana (24/7) kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2023.
Septemba 29, 2023, akitangaza kwa niaba ya Serikali kuanza kwa ratiba LATRA ilishiriki katika zoezi la kufanya maandalizi ya kuanza kwa safari za usiku kwa kushirikiana na wadau wake muhimu, hasa wamiliki wa mabasi (wakiwemo
TABOA) na ilitekeleza maamuzi ya Serikali kwa kuanza kutoa ratiba za mabasi kusafiri usiku na mchana (24/7) kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2023.
Aidha, tathmini ya LATRA ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa ruhusa hii ya safari za
usiku na mchana (24/7) umeonesha Wananchi wengi wamefurahishwa na kuridhishwa na maamuzi ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.
Dkt Samia Suluhu Hassan kuondoa zuio la mabasi kusafiri usiku. Aidha, kun mwitikio mkubwa wa Wananchi kutumia usafiri wa usiku kuliko mchana, na msongamano wa abiria kwenye Stendi umepungua sana, na ‘mchezo’ wa mabasi kukimbizana umepungua sana na unaelekea kwisha kabisa.
Vilevile, tathmini ya LATRA inaonesha kuwa safari hizi za 24/ zimepunguza gharama za njiani kwa abiria na kuboresha matumizi ya muda wao kwenye shughuli za
kiuchumi, kijamii na kujiongezea vipato.
Usafirishaji kwa njia ya reli nchini ni mojawapo ya eneo
linalodhibitiwa na LATRA kwenye maeneo ya usalama wa miundombinu na mabehewa, nauli, viwango vya ubora na ufanisi wa utendaji.
Katika hatua ya kutimiza majukumu haya, LATRA katika kipindi kinachoanzia Februari, 2021 hadi
Machi, 2025 imefanya jumla ya kaguzi 275 katika miundombunu, ishara na mawasiliano, vitembea reli (vichwa na mabehewa) na uendeshaji. Kati ya kaguzi
hizi, 143 nilikupa kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), na kaguzi 132 zilikuwa kwaMamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
4.2.2 Uanzishwaji wa Huduma za Treni za SGR Sambamba na hayo katika maandalizi ya kuanza kwa huduma za usafiri wa abiria kwa treni za SGR, LATRA ilikuwa na jukumu la kuthibitisha ubora wa vitembea relik kabla ya kuanza kutoa huduma.
LATRA iliungana na timu ya wataalamu wa TRC na Wizara ya Uchukuzi kwenda Nje ya Nchi (zilikokuwa zinaundwa) na kukagua na kuthibitisha.
Jumla ya vichwa vya treni 17, Mabehewa ya abiria 56, treni za seti za umeme (EMU) 10 na Mabehewa ya mizigo 264 yamekaguliwa kipindi cha uundwaji katika nchi za Korea, China, Malaysia na Ujerumani.
Pia Mamlaka imefanya kaguzi za majaribio kwa mabehewa na vichwa hivyo baada ya kuwasili nchini kabla ya kuanza kutumika kutoa huduma.
Alisema kwamba mwaka huu wa fedha 2024/2025 LATRA imejipanga kuhakikisha kuwa huduma
za usafiri ardhini kwa abiria, mizigo na wa kukodi zinakuwa bora na salama zaidi,
zinawafikia wananchi, kuondoa kero na changamoto mbalimbali katika sekta.
![]() |
No comments:
Post a Comment