TUTASHIRIKI KIKAMILIFU UCHAGUZI MKUU 2025 - MASSANZA - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Saturday, April 26, 2025

TUTASHIRIKI KIKAMILIFU UCHAGUZI MKUU 2025 - MASSANZA


NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Kigoda cha Vijana Taifa wa chama cha National League for Democracy (NLD), Sabra Massanza, ametangaza dhamira ya vijana wa chama hicho kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kwa lengo la kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele katika uamuzi wa hatma ya taifa lao.


Akizungumza katika mahojiano maalum kupitia kipindi cha Morning Kiss Weekend kinachorushwa na Kiss FM 98.9, Ndugu. Massanza amesema:


 “Chini ya uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Vijana wa NLD Taifa, tutashiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 2025. Bila ushiriki wetu na bila kupata nafasi za kuwasemea vijana wenzetu na kusukuma mbele Ajenda za Vijana, ni nani atasikia sauti zetu ndani ya nchi hii?”


Mbali na ushiriki wa kisiasa, Massanza amesisitiza wajibu wa vijana katika kulinda amani na mshikamano wa kitaifa.


 “Vijana, ni wajibu wetu pia kulinda amani na utulivu wa taifa letu. Hakuna nchi iliyopata maendeleo ikiwa na machafuko. Kwa hivyo basi, ni wajibu wetu kuilinda amani ya nchi hii kwa wivu mkubwa sana. Tuilinde amani yetu kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi, na baada ya uchaguzi.”


Katika hitimisho lake, Massanza alinukuu kaulimbiu ya chama cha NLD. “Uzalendo, Haki na Maendeleo”, akibainisha kuwa nguzo hizo zote zinaanzia na Amani kama msingi wake.

No comments:

Post a Comment