MWANADADA Tatu Songoro ambaye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Udiwani Viti Maalumu Wilaya ya Ubungo.
Kada huyo ambaye ni mkazi wa Saranga, Kata ya Kimara Jimbo la Kibamba ametumia fursa kama kijana kuwania nafasi hiyo ili kutimiza malengo ya wananchi wa Kata hiyo.
"Nimejitokeza kuchukua fomu leo, Juni 29, 2025 baada ya kujipima na kuamini kuwa naweza hivyo tusubiri jina likirudi na kampeni kufunguliwa nitasema mengi, itoshe kusema nimekuja kuchukua fomu basi," amesema.
No comments:
Post a Comment