Na Charity James
SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa nchini (BFT) limesema kwasasa linaelekeza nguvu zake katika utendaji zaidi kwa
ajili ya kuandaa programu za mwakani.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana Katibu Mkuu BFT Makole Mashaga alisema wamekamilisha kila
kitu mwaka huu na wanachosubiri kuanza kwa mwaka mpya ili ratiba yao kwa ajili ya mwaka ujao ianze kufanya
kazi.
"Tupo kiutendaji zaidi ikiwani pamoja na kugawana majukumu baina ya viongozi kwa lengo la kuhakikisha
mwakani tunapata mafanikio makubwa na kutimiza malengo tuliyojiwekea," alisema.
Alisema baadhi ya malengo ya mwakani ni pamoja na kuhakikisha linainua mchezo huo kwa upande wa
wanawake nchini ambao wameonekana kuwa nyuma katika mchezo huo.
Pia alichukua fulsa hiyo kuwaomba wasichana kujitokeza kujiunga katika mchezo huo ili kuweza kupata timu bora
itakayowakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Saturday, December 17, 2011
New
Wasichana waombwa kujitokeza kwenye masumbwi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment