Na Asha Kigundula
TIMU ya soka ya Yanga itacheza mechi tatu za kirafiki
kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara inayoanza
kutimua vumbi Januari 23 mwakani.
Akizungumza na Jambo Leo jana Ofisa Habari wa Yanga
Louis Sendeu, alisema kuwa kabla ya kuanza kwa Ligi
watacheza mechi tatu kubwa kama maandalizi ya mechi.
Sendeu alisema kuwa mechi hizo ni moja ya program za
kocha wao Mkuu Kostadin Papic, ikiwa ni kutaka kujua
kikosi chake kabla ya kuanza kwa mzunguko huo.
Alisema mpaka sasa bado hawajajua ni lini watacheza
mechi hizo lakini wapo katika harakati ya kuendelea
kutafuta mechi nzuri kwa ajili ya kuipa timu yao mazoezi.
Sendeu alisema timu yao ipo katika mazoezi makali kwa
ajili ya maandalizi ya kutetea ubingwa wao ambao
waliuchukua msimu uliyopita.
Saturday, December 17, 2011
New
Yanga kuicheza mechi tatu za kujima nguvu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment