Na Asha Kigundula
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kinasaka wadhamini kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi utakaozikutanisha timu za Taifa za Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' dhidi ya Zanzibar, utakaofanyika Disemba 31 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Akizungumza na Jambo Leo kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari wa ZFA, Munir Zakaria, alisema mpaka sasa hawajapata wadhamini wa mashindano hayo, ikiwa ni pamoja na mechi ya ufunguzi.
Alisema wanaendelea kuwasiliana na makampuni mbalimbali yaweze kusaidia kudhamini mechi hiyo na mashindano kwa ujumla.
Alisema licha ya kufanyika kwa mechi hiyo ya ufunguzi, kutakuwa na mechi za hatua ya makundi na baadae hatua ya nusu fainali na fainali ambayo itafanyika Januari 12 Pemba siku ya kilele cha sherehe za Mapinduzi.
Alisema katika mashindano hayo, jumla ya timu nane zitashiriki,ambapo timu tatu zinatoka Tanzania Bara na tano visiwani humo.
Zakaria alisema timu zinazotoka Tanzania Bara ni mabingwa watetezi, Simba, Yanga na Azam FC.
Kundi A kuna timu za Miembeni, KMKM, Jamhuri ya Pemba na mabingwa watetezi Simba, wakati Kundi B kuna timu za Azam FC, Mafunzo, Kikwajuni na Yanga.
Katika fainali za mwaka jana, Simba ilikutana na Yanga na kufungwa kwa mabao 2-0, mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Amaan.
Saturday, December 17, 2011
New
ZFA yasaka wadhamini wa Mapinduzi Cup
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment