- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2013

Azam kuweka kambi Sauzi
Na Charity James
KLABU ya Azam FC, inatarajia kuweka kambi Afrika Kusini kujiandaa kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu unaokuja.
Azam inatarajia kaunza kambi yake Juni 24, mwaka huu  kwa sasa wachezaji wako likizo.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Meneja Msaidizi wa timu hiyo, Jemedari Said alisema kwa sasa wachezaji wapo mapumzikoni na kwamba wanatarajia kuanza mazoezi Juni 24.
Alisema ukiachana na timu kuanza kambi kwa ajili ya msimu ujao lakini pia wanatarajia kuweka kambi Afrika Kusini lakini bado haijajulikana ni lini watakwenda.
kocha wa Azam Fc, Stewart Hall
Akizungumzia usajili kwa wachezaji katika msimu ujao, alisema bado hawajapata ripoti kutoka kwa kocha na kwamba akihitaji mabadiliko basi itafanyika hivyo.
“Kawaida timu yetu haifanyi usajili kwa matakwa ya viongozi la hasha!tunasajili kutokana na mahitaji ya mwalimu, hivyo tunasubiri ripoti kutoka kwa mwalimu na ikionesha kuwa na mapendekezo ya kufanya usajili kwa baadhi ya maeneo tutafanya hivyo," alisisitiza Said.
Timu hiyo ambayo inaonekana kuleta mageuzi katika soka la Tanzania, misimu miwili iliyopita imefanya vizuri na kuzishangaza timu kubwa za Simba na Yanga kwa kushika nafasi ya pili.
Mbali na kuiwakilisha nchi kwa mara ya pili mfululizo katika michuano ya Kombe la Shirikisho ni timu pekee nchini kwa msimu uliopita kufika katika mzunguko wa pili katika michuano ya kimataifa.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam nusura itinge hatua ya mtoano ya michuano hiyo baada ya kufungwa na FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1.
Kabla ya hapo Azam ilizifunga timu za Al Nasri Juba ya Sudan Kusini na Barrack Young Controllers ya Liberia.

No comments:

Post a Comment