Fidodido ajipanga kuipua kitu kipya - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2013

Fidodido ajipanga kuipua kitu kipya


Na Hamisi Magendela
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Edward Hamisi 'Fidodido' amesema yuko katika hatua za mwisho kukamilisha wimbo ambao bado hajaupa jina.
Akizungumza Dar es Salaam jana , Fidodido alisema ngoma hiyo imetengenezwa na Prodyuza Mensen Selector.
Fidodido
"Naamini ngoma hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali kama zilivyokuwa nyingine zilizotangulia na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huu ambao umejaa changamoto nyingi," alisema Fidodido.
Msanii huyo alisema kuwa wimbo huo unatarajiwa kuachiwa mwezi ujao pindi utakapokamilika.
Hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuhakikisha wanamuunga mkono katika kazi hiyo na ijayo kama walivyofanya kwa zilizotangulia.

No comments:

Post a Comment