Jike la Chui kutoka kivingine - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2013

Jike la Chui kutoka kivingine


Na Hamisi Magendela
MWANADADA wa mipasho Hanifa Maulid 'Jike la Chui' amesema kuwa yuko katika hatua za mwisho kutambulisha kazi mpya siku chache zijazo ambao utakuwemo katika albamu yake ya kwanza.
Akizungumza Dar es Salaam jana Jike la Chui alisema anaamini kibao hicho kitakuwa na ubora wa aina yake kama kilivyokuwa alichokiachia siku chache zilizopita cha Makavu Live.
 "Wimbo wa Makavu Live umeniweka mahala pazuri naamini unaofuata ambao nitauachia siku chache zijazo utaniweka katika ramani nyingine zaidi kwenye muziki wa taarabu," alisema Jike la Chui.
Msanii huyo alisema albamu yake inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ambayo itakuwa ya kwanza katika maisha yake ya muziki huku akiweka historia nyingine kwenye tasnia hiyo.
Anafafanua kuwa mchakato wa kuachia wimbo huo na albamu ni hatua ya mafanikio katika maisha ya muziki huo huku akiamini kuwa ni sehemu ya kujiongezea kipato.
Msanii huyo licha ya kufanya kazi kivyake na kung'ara pia yuko katika kundi la King's Moden Taarabu lililo chini ya Mkurugenzi wake, Hamisi Majariwa 'Kijoka'.

No comments:

Post a Comment