Jaydee amlilia Mangwea, asogeza mbele tamasha - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2013

Jaydee amlilia Mangwea, asogeza mbele tamasha


Na Zahoro Mlanzi
MSANII mkongwe wa miondoko ya Bongofleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee', amesema kutokana na kifo cha mwanamuziki wa hip hop Albert Mangwea 'Ngwea , amesogeza mbele uzinduzi wa albamu yake mpya ya 'Nothing but the trust', mpaka atakapotangaza tena.
Msanii, Lady Jaydee
Akihojiwa na Kituo cha Redio cha East Africa kupitia kipindi cha Super Mix, Jaydee jana alisema ameahirisha kufanya uzinduzi huo uliopangwa kufanyika kesho Nyumbani Lounge kutokana na  ukubwa wa msiba huo.
Nyota huyo alipotakiwa kumzungumzia jinsi anavyomfahamu Mangwea, alisikika akizungumza kwa huzuni huku akilia na kushindwa kuendelea.
Jaydee alikuwa katika maandalizi ya mwisho ya uzinduzi wa albamu hiyo ambao ungefanyika Mei 31, mwaka huu ambao ungekwenda sanjari na kusherehekea kutimiza miaka 13 akiwa katika muziki.

No comments:

Post a Comment