Mwandishi Wetu
ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, George Mpondela amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya ugonjwa wa moyo uliyokuwa yakimsumbua.
Marehemu Mpondela alifariki dunia jana baada ya kulazwa katika Hospitali hiyo kwa muda wa wiki tatu katika wodi ya maradhi ya moyo,mwili wake unatarajiwa kusafishwa kesho kwenda kijijini kwao Misha Wilaya ya Tabora vijijini, mkoani Tabora kwa maziko.
Kabla ya mwili wake kusafirishwa utaagwa katika hospitali ya hiyo kuanzia saa 2 asubuhi siku hiyo na baada hapo taratibu za kuusalifishwa kwenda mkoani Tabora kwa maziko zitaanza.
Enzi za uhai wake marehemu aliwahi kuiongoza Yanga mwaka 1993 alipochaguliwa kwa kishindo kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani akiwa chini ya wake Mwenyekiti, Dk. Jabir Katundu.
Marehemu Mpondela alizaliwa kijiji cha Misha, Tabora, Septemba 28 mwaka 1942 na kipindi kirefu cha maisha yake alikuwa mtumishi wa Mamlaka ya Pamba Tanzania.
Marehemu ameacha mke na watoto tisa, ambao ni Pius, Robert, Hilton, Kennedy, Joseph, Collin, na wa kike Linda, Jaqcueline na Jennifer. Mungu aileze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amin.
Kwa hisani ya BIN ZUBEIRY BLOG
No comments:
Post a Comment