Magendela Hamisi
MGOMBEA wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba, Michael Wambura amezidi kukalia kuti kavu baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutarajia kumhoji Jumanne wiki ijayo.
Taarifa zilizopatikana Dar es Salaama jana kutoka ndani ya Shirikisho hilo zilibainisha kuwa Wambura anatarajiwa kuitwa siku hiyo ili kuhojiwa kutokana na maneno aliyozungumza juzi katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Wambura katika mkutano wake na waandishi wa habari aliwataka baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono kwenda katika matawi ya klabu hiyo kuhamasisha habari nzuri bila kufafanua habari nzuri ni zipi.
Pia inadaiwa kauri za aina hiyo katika mkutano huo ndizo zitakazomweka njia panda katika harakati zake za kuwania nafasi ya uraisi wa Simba ambao unatarajiwa kufanyika Juni 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Awali Wambura aliondolewa kuwania nafasi hiyo na Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba iliyochini ya mwanasheria Damas Ndumbaro baada ya kudaiwa kukiuka Katiba ya klabu kwa kuipeleka mahakamani.
Moja ya kipengele katika ya klabu hiyo inadaiwa kusema kuwa mwanachama ambaye amesimamishwa uanachama hana haki ya kushiriki katika shuguli za Simba kwa mujibu wa ibara ya 12 (3) ya katiba ya hiyo mwaka 2010 na ibara ya 12 (3) ya katiba ya Simba ya mwaka 2014.
Baada ya Kamati ya Ndumbaro kutoa maamuzi hayo ya kumuengua, Wambura alikimbilia TFF kupinga hatua hiyo katika Kamati ya Rufani ya TFF iliyochini ya mwanasheria, Julius Lugaziya.
Kamati hiyo baada ya majadiliano ya siku mbili ikaamuru Wambura arejeshwe katika kinyang'anyiro hicho hali iliyofanya wanachama wa Simba kuganyika makundi mawili wengi wakiunga mkono na wengine wakipinga.
Hivyo macho na masikio ya wadau wa michezo na wanachama wa Simba kwa sasa yapo katika Kamati Maadili ya TFF, kusubiri kitu gani kitaamuliwa baada ya kumuhoji, Wambura siku hiyo ya Jumanne wiki ijayo.
cIOOO
Saturday, June 14, 2014
New
Wambura kikaangoni tena TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment