Patrick Kluivert, Aliikacha Ajax FC kwa kashfa ya ubakaji - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, June 14, 2014

Patrick Kluivert, Aliikacha Ajax FC kwa kashfa ya ubakaji

PATRICK Kluivert mwandanda aliyezaliwa Julai Mosi mwaka 1976 katika mji wa Amsterdam nchini Uholanzi ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa kulipwa alistaafu soka akiwa na mabao 200.
Mchezaji wa zamani wa NewCastal United alianza kujifunza kusakata mpira wa miguu katika mitaa ya mji wa Asterdam Uholanzi kabla ya kujinga katika klabu ya Schellingwoude.

Baada ya kuonesha kiwango kizuri alijiunga na klabu ya vijana ya Ajax FC wakati huo akiwa na umri wa miaka saba na katika kipindi hicho alikuwa akicheza namba tofauti ikiwemo ya ulinzi.

Katika kipindi hicho alionesha ukakamavu, utaalamu na alikuwa akitumia akili sanjari na kasi kubwa anapokuwa uwanjani hali iliyofanya wadau wa soka kuvutiwa naye.Kluivert baada ya kuonesha uwezo na umaridadi napokuwa uwanjani alifanikiwa kuanza kuchezea timu ya taifa ya vijana chini ya mika 15 hadi 17 kwa mafanikio makubwa.

Aina ya uchezaji wa KluivertKluivert ni mchezaji mrefu na mwenye uwezo wa kuchezesha miguu kwa haraka ili kumchanganya adui yake na mwepesi kurudi katika namba anayocheza ili kuimalisha ngome yake.Mara nyingi ufananishwa na Ronaldo,pia naposhambulia hurudi haraka kusaidia nafasi ya ulinzi.

Mchezaji huyo ni sehemu vizazi vya dhahabu katika miaka ya 90 kilichotengenezwa na timu ya Ajax kabla ya kuanza kuicheza timu ya wakubwa.August 21, mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 18 alifanikisha timu yake kupata ubingwa wa 'Dutch Super Cup' dhidi ya timu ya Feyenoord ambako alishinda bao la kwanza.

Katika msimu wa mwaka 1994/95  alikuwa katika kiwango kizuri akiwa na timu ya vijana ya Ajax hali iliyofanya kuchaguliwa kuwemo katika kikosi cha wakubwa akiwa na  Edgar Davids, Clarence Seedorf na Edwin van der Sar kufanikiwa kubeba kombe la kombe la Uefa.Kluivert akitokea benchi katika dakika ya 85 katika fainali dhidi ya A.C.

Milan uliochezwa mjini Vienna nchini Austria na baada ya mchezo huo kumalizika akaitwa "Golden Boy" na kuiweka Ajax katika mstari wa mbele.Baada ya mwaka mmoja akasajiliwa na Milan na kumkia Bosman kwa mkataba mpya kwa mwaka 1997 na wakati huo alikuwa amefunga mabao 39 katika michezo 70 aliyoicheza kiwa nchini Uholanzi kwa misimu mitatu.

Akiwa Milan alinza vema baada ya kufunga bao dhiti ya wapinzani wao.Juventus katika mchezo wa kirafiki na baada ya kushinda mabao sita tu katika ligi ya Serie A,aliamia katika timu ya Barcelona FC ya Ispania inayoshiriki ligi ya La Liga.August, 28 mwaka 1998, ikiwa imesalia saa moja kabla ya kufungwa muda wa uhamisho, mchezaji huyo alisaini mkataba wa miaka minne ya kuitumikia timu hiyo.

Alisani Barcelona kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 8.75 million na kufanikiwa kuwa na uhusiano mzuri wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil,Rivaldo Ferreira.Wakiwa katika timu hiyo walicheza kwa mafanikio makubwa katika kipindi cha msimu wa mwaka 1998/99 japo kikosi hicho hakikufanikiwa kubeba ubingwa wa nchi hiyo baada ya kushika nafasi ya tatu.

Pia katika msimu huo Kluivert alifanikiwa kufunga mabao 15 na katika kipindi cha majira ya joto aliachana na kikosi hicho na kutua nchini Uingereza katika klabu ya Newcastle United.Alijiunga na Newcastle United Julai 21, mwaka 2004 na akiwa ameitumia Barca kwa kipindi cha miaka sita na kuifungua mabao 90 na kwa kipindi chote kuwa kinara wa mabao katika ligi hiyo ya La Liga.

Kutua Newcastle United

Kluivert alijiunga katika kikosi cha Newcastle United kikiwa na Alan Shearer na kumaliza msimu huo akifunga mabao 13 na baada ya kuitumikia baada ya miaka miwili akarejea tena nchini Ispania katika klabu ya Valencia.

Akiwa katika timu hiyo mpya alipata maumivi akiwa na ameichezea timu dakika 202 na kufanya kutumia msimu huo vibaya kwa kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu hali iliyomfanya kupoteza muelekeo wa ufanisi wake uwanjani.

Baada hapo akaenda kufanya majaribio katika timu ya PSV na wakati kukawa na tetesi kuwa anahitaji kurejea katika timu yake ya nyumbani ya Ajax FC na kufanikiwa kusaini kwa mwaka mmoja katika timu hiyo ya PSV.

Akiwa na PSV alifanikiwa kujikokota vema na katika mchezo dhidi ya Feyenoord na katika mchezo huo walifanikiwa kushinda mabao 2-1 huku mchezaji huyo akicheza kimoja baada ya kuumia tena na kutolewa.

Hakika kutokana na kuwa majerui kiwango cha mchezaji huyo kikaanza kuporomoka na katika mchezo uliowakutanisha dhidi ya timu yake ya zamani ya Ajax , mchezaji huyo hakuwa na furaha baada ya kuifunga timu hiyo mchezo uliochezwa katika uwanja wa Philips.

Julai 25, mwaka 2007, Kluivert alipata ofa ya kufanya majaribio katika klabu ya Sheffield na baadaye akabadilisha upepo na kwenda nchini Ufaransa kujiunga na klabu ya Lille na kutoa mchango mkubwa katika kikosi hicho.

Kutokana na kuonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata soka lakini akawa anaangushwa na kuwa majeruhi, meneja wa timu hiyo Claude Puel alimpa ushauri wa kubadili muelekeo wa kuwa kocha badala ya kuendelea kucheza soka.

Baada ya kupewa mawazo hayo, Aprili 29 mwaka 2008, Vyombo vya habari nchini Uholanzi walianza kuripoti kuhusu habari za Kluivert kuamua kujiunga na kozi ya ukocha wa mpira wa miguu iliyokuwa ikiendeshwa na chama cha mpira cha nchi hiyo kinachoitwa Dutch Football Association (KNVB).

Baada ya kupita katika timu mbalimbali baadaye akawa kocha mchezaji wa timu ya N.E.C., na katika msimu wa mwaka 2011/12 akawa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 20 na August mwaka 2012, Kluivert  akawa msaidizi katika kikosi cha timu ya taifa Netherlands akiwa chini ya kocha, Louis van Gaal.

Pia ikumbukwe Kluivert akiwa mchezaji wa timu ya taifa katika mashindano ya Ulaya mwaka 1996 alikosa baadhi ya michezo ya fainali hizo kutokana na kuwa majeruhi na wakati timu yake ikicheza mchezo wa mwisho wa makundi aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Dennis Bergkamp na kufunga bao dhidi ya Uingereza.

Kutokana na kuiwezesha timu yake kupata ushindi aliiwezesha kuvuka hatua hiyo kwa tofauti ya mabao dhidi ya timu ya Scotland ambao walipoteza ushindi baada ya kupigiana penalti dhidi ya Ufaransa.

Pia katika kipindi cha michuano ya Ulaya ya mwaka 2000,Kluivert alifunga  hat-trick katika mchezo dhidi ya Yugoslavia baada ya kuwafunga mabao 6-1 na kuwaondoa katika mashindano hayo .

Katika michuano hiyo, Kluivert akawa mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne na kutinga hatua ya nusu fainali dhidi ya Italia na kuondelewa kwa mikwaju ya penalti na katika mchezo huo mwanandinga huyo akawa miongoni mwa waliokosa penaliti.

Licha ya kutolewa katika fainali hizo, mwanasoka huyo hadi leo anakumbukwa kufanya vizuri katika michezo ya nyumbani na kufanikiwa kupata kiatu cha dhahabu na baadaye katika mashindano ya Ulaya ya mwaka 2004 alipata umaarufu mkubwa akiwa amevaa jezi namba tisa ya nchi yake.

Katika michezo ya kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2006 kocha, Marco van Basten hakumwita mchezaji huyo kuitumikia kikosi hicho kutokana na kuwa majeruhi ya muda mrefu.

Kabla ya kuiwa majeruhi mwanadinga huyo alikuwa tegemo kwa timu yake ya taifa kwa kuifungia mabao mahimu na katika kipindi chote alipokuwa akiichezea timu ya taifa alifanikiwa kuifungia mbaoa 40 kabla ya ujio wa mchezaji Robin van Persie in 2013.

Maisha kwa ufupi
Mwaka 1995 alihukumiwa kuitumikia jamii saa 240 baada ya kupatikana na kosa kusababisha ajali, iliyosababisha Mkurugenzi wa kitengo cha Upasuaji wa moja ya hospitali nchini humo kupoteza maisha.

Licha ya hukumu hiyo kutolewa lakini vyombo vingi vya habari nchini humo vilikosoa hukumu hiyo ambayo pia ilimhukumu kwa kumpiga marufu kuendesha gari. Na mwaka 1996 mwandinga huyo aliyezaliwa siku moja na mchezaji  Ruud van Nistelrooy alikutwa na kashfa ya kubaka.

Tuhuma hiyo ndiyo iliyokuwa sababu kuondoka kwake katika kikiosi cha timu ya soka ya Ajax FC, lakini hakiweza kuthibitishwa na kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani jambo ambalo lilionekana kumchafua mchezaji huyo na kuchukizwa na hilo na kuamua kuachana na klabu hiyo na kutua AC Milan.

Septemba 24, mwaka 2007, mkewe anaeitwa, Rossana Lima alijifungua mtoto wa kiume anaeitwa, ShanePatrick. Kwa sasa mchezaji huyo wa zamani wa New Castle United ana watoto wanne wa kiume, watatu alizaa na mkewe wa kwanza ambao ni Quincy, Justin na Ruben.

Imeandaliwa na Magendela Hamisi kwa msaada wa mitandao ya Habari

No comments:

Post a Comment