Sababu za uchafu kwenye via vya uzazi - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, June 14, 2014

Sababu za uchafu kwenye via vya uzazi


Magendela Hamisi

NI siku nyingine tena ya Jumapili wa tulivu ninaamaanini wapo ambao wanatoka kanisani na wengine wamepumzika baada ya shughuli za utafutaji ya wiki nzima wakitafakati ni jinsi kesho Jumatatu wataanza wiki nyingine kwa ajiri kuimairisha uchumi na kuinua kipato.

Wakati kila mmoja akitafakari namna ya kujinasua katika hali hiyo ni vema pia tukarejea katika changamoto za afya kwa mwanamke na leo nikijikita zaidi katika suala la utokaji majimaji au ute katika viungo vya uzazi, tatizo ambalo limekuwa likiwakabiri baadhi ya wanawake na wasichana.
 
Tatizo la utokaji majimaji au ute katika via vya uzazi vya mwanamke ni jambo la kawaida wakati ambao bado ana umri wa kuzaa ikiwa ni sehemu ya mwili kuondoa sumu.

Ute huu kwa kawaida huwa hauna rangi, hadi ukiwa umekauka juu ya nguo ya ndani ndio huashiria rangi nyeupe au njano. Pia huwa ni kiasi kidogo ambacho hakihitaji mwanamke kuvaa kitu kingine zaidi ya nguo ya ndani ya kawaida ili kuuzuia.

Majimaji hayo (ute) wakati mwingine yanaweza kuashiria ugonjwa wa hatari yanapokuwa yanaambatana na dalili mbalimbali na kutoa harafu mbaya.

Hali ya mwanamke kutokwa na majimaji (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya.

Endapo majimaji (Ute) huo mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili.

Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaosababisha magonjwa ukiwemo wa Vaginosis.

Pia majimaji hayo huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin's glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku. Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi.

Wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.

Ikiwa ute ute huo unabadilika rangi na kuwa kama maziwa mtindi, rangi ya kahawia, njano, kijani, rangi ya usaha na au rangi ya juisi ya parachichi hilo ni tatizo.

Pia majimaji hayo yakiambatana harafu na kali na hata kama mwanamke akiwa ameoga na kuvaa vizuri inakuwa kama shombo la samaki na hasa wakati wa kushiriki tendo la ndoa na baada.

Kwa mujibu wa matabibu, dalili nyingine ni ute kuzidi kiwango chake cha kawaida cha kila siku (abnomal quantity of discharge), maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa sanjari na wakati wa kujisaidia haja ndogo.

Pia kuwashwa sehemu za nje na ndani za via vya uzazi vya mwanamke pamoja na via vya uzazi /uke kuwa mwekundu kuliko rangi yake ya ngozi ya siku zote ni dalili mojawapo za tatizo.

Muwasho sehemu za mlango wa uke na kwa ndani, maumivi chini ya kiuno mbele na nyuma na pia chini ya kitovu na hasa kushoto na kulia ni dalili mojawapo.

Pia sehemu ya nje (vulva) ya via vya uzazi kuwa nyekundu na wakati mwingine wekundu kuambatana na michubuko, vidonda na maumivu zinaonesha hali ya ugonjwa.

Sababu za ugonjwa
Sababu kutokwa na majimaji hayon hasa yale yenye dalili za ugonjwa ni maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa ya Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis bacteria.

Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili, hivyo ni vema kukawa na uangalifu mkubwa wakati matumizi ya vifaa hivyo kwa kipindi hicho ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza baada ya hapo.

Anasema kuwa maambukizo katika njia ya uzazi ya mwanamke na si njia ya mkojo ambapo anabainisha kuwa hii hutokana na kufanya mapenzi yasiyo salama na mtu ambaye ana magonjwa ya zinaa hivyo bakteria, virusi ama fungus wanashambulia njia ya uzazi.

Sababu nyingine ni usafi wa sehemu za siri usiozingatiwa wakati hedhi nayo ni moja ya kinachoweza kusababisha mazalia ya bacteria na baadaye kuanzisha tatizo kwa muhusika.

Pia mambukizi hayo yapo ya aina kubwa tatu ambayo kitaalamu ni bacterial Vaginosis, Trchomoniasis na Monilia pamoja na inaelezwa kuwa kufanya ngono kinyume cha maumbile na wakati huo huo kuhamia kwenye uke, usababisha kuhamisha uchafu na wadudu wanaoshambulia njia ya uzazi.

Sababu nyingine inayosabisha hayo ni chakula kilichojaa mafuta kinachochea/kinaamsha seli za mafuta (fat cells) mwili mzima na uchangia kuzalishwa kwa homoni nyingi za 'estrogen'.

Homoni hizo zikiambatana na upungufu wa 'fiber' zinachochea ukuaji wa bacteria wa ndani ya utumbo kwa kitaalamu wanaitwa 'Clostridia' ambao wanasifa ya kubadilisha 'bile acid' kuwa homoni za estrogen ambazo zinapozidi husababisha tatizo la mwanamke kutokwa na uchafu katika via vyake vya uzazi.

Pia kutumia vidonge vya uzazi wa mpango bila ushauri wa mtaalamu usababisha kuharibu ukuta wa uke (mucus membranes of the vagina)ambao ni ulinzi, hivyo huharibu afya ya uke kwani huufanya uwe na hali ya 'alkali' hali ambayo huruhusu/uchochezi bacteria na fangasi kuvamia na kuzaliana kirahisi.

Uchafu wa mavazi na uchafu wa mwili hasa kwa mwanamke ambaye hajui jinsi ya kujisafisha katika via vyake vya uzazi ili kuondoa seli zilizokufa (dead cells) na kushiriki tendo la ndoa bila kinga.

Mojawapo ya athari za kutokwa na uchafu ukeni ni ugumba ambao hutokea maambukizi yanapofika kwenye mirija na kuleta uvimbe ambao huziba au kusababisha kutengenezwa kwa maji machafu mazito ambayo nayo huziba mirija na huua mimba kila inapotungwa.

Kuvimba kwa mirija ya uzazi ambapo kitaalamu tatizo hili hujulikana kwa jina la Salpingitis. Likichelewa kutibiwa mirija huziba na hivyo mwanamke hupoteza uwezo wake wa kushika ujauzito.

Tiba

Namna ya kujitibu tatizo la utokwaji wa uchafu nyumbani kabla ya kutafuta tiba hospitalini
kinachotakiwa ni kuacha kutumia sukari na vyakula/vinywaji vyenye sukari kwa muda wa miezi miwili kwani fungus kama candida albicans hutumia sukari kama chakula.

Kutumia karafuu ya unga kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto na asubuhi na jioni kila siku kwa miezi miwili, kutumia juisi ya karoti kila siku asubuhi na jioni glasi moja kwa miezi miwili.

Kuacha kunywa maziwa kwa miezi miwili au zaidi kutumia mchuzi wa kabeji ambao hauna kiungo chochote kunawia katika via vya uzazi.

Ni muhimu mwanamke akifanya haya yote na bado haoni mafanikio, atafute tiba ya ziada haraka ili kuepuka ugumba.

Tahadhari ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.

Namna ya kujikinga

Wanapaswa kuvaa nguo za pamba na kuachana na za nailoni ambazo huleta joto jingi na unyevunyevu usiohitajika katika via vya uzazi pamoja na kujisafisha kutoka  kwenda nyuma na si nyuma kwenda mbele.

Pia kuachana na mafuta ya kulainisha kuta za uke bila kufuata ushauri wa daktari, kuacha kushiriki tendo kinyume cha maumbile na kuepuka milo yenye mafuta na kupunguza ulaji wa nyama nyekundu.

Baada ya kuanza matibabu ni kusitisha tendo la ndoa hadi tiba ikamilike na kwa mafanikio, pia muhusika aepuke kukuna maeneo  yanayowasha kwani anaweza kusababisha mwasho zaidi.

Mwandishi wa makala safu hii, si daktari wala muuguzi, yaliyoandikwa yametokana na tafiti,mitandao na wataalamu wa Afya.Shukrani ziende kwa Dk. Simoni Rusigwa wa kliniki ya Sure Herbal kwa ushikiriano wake hadi kukamilisha makala hii.

magendela@gmail.com

1 comment: