TPBC kufanya mkutano kesho - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, June 14, 2014

TPBC kufanya mkutano kesho



Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), kesho litafanya mkutano wake mkuu kwa ajili ya kuimarisha mchezo wa ngumi.

Akizungumza na magendela blog, Katibu Mkuu wa TPBC, Hamis Kimanga, alisema kuwa mkutano huo mkuu utafanyika kwenye Ukumbi wa DDC Keko, Dar es Salaam.

Kimanga alisema lengo la mkutano huo ni kuondoa ufa uliopo katika mchezo wa ngumi na wadau kuwa kitu kimoja.

Alisema katika mkutano huo wanaomba wadau wajitokeze kwa wingi ili waweze kurudisha mchezo huo wa ngumi.

Kimanga alisema kuwa wanachama wote wajitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanafanya marekebisho ya marekebisho ya Katiba.

Alifafanua kuwa TPBC ina viongozi 15, ambapo viongozi wa juu ni watano na wajumbe 10,
ikiongozwa na Mwenyekiti wake Chaurembo Palasa,  Katibu Hamisi Kimanga, Makamu Mwenyekiti Chuku Duso na Katibu msaidizi Busato Michael.

Kimanga aliongeza kuwa katika kuhakikisha wanarudisha mchezo huo kama ulivyokuwa zamani wanapanga mikakati imara ili kuboresha.

Kimanga alisema kuwa TPBC imeshafanya Semina ya waamuzi na majaji wiki iliyopita na kupata waamuzi 11.

"Tunaomba wadau wote wa ngumi waudhurie mkutano mkuu ili tuendeleza ngumi zirudi ambazo kwa sasa imefika wakati tuwe tunakaa na kukubaliana na sio kugeuza mchezo wa
ngumi kama genge la watu kugombana na kuwapa nafasi wasio wadau wa mchezo huo kusimamia"alisema.

No comments:

Post a Comment