Asha Kigundula
JUMLA ya warembo 30 wa shindano la Redd's Miss Tanzania wameingia kambini kwa ajili ya fainali za
shindano hilo zitakazofanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika hafla maalumu ya kupokea warembo hao, Mkurugenzi wa shindano hilo
Hashim Lundenga, alisema kuwa warembo hao wataweka kambi yao kwenye Hoteli ya JB Bermont,
iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Aliweka wazi kuwa wanyange hao watakuwepo hapokwa muda wa siku tatu kwa ajili ya semina ya
kutambuana na kufahamishwa miiko ya kambi na baada ya hapo watatembelea vivutio vya utalii
vilivyopo nchini.
Lundenga alisema vivutio watakavyotembelea ni vilivyoko katika mikoa ya Morogoro, Arusha na
Kilimanjaro na baada ya kumaliza ziara hiyo watarembelea Dar es Salaam kwa ajili ya ratiba nyingine.
Warembo waliyoingia kambini mwaka huu ni Sofia Maey kutoka Singida, Lilian Timothy (FM DSM,
Junes Ndalima (Ustawi wa Jamii, DSM) na Martha John (Iringa).
Wengine ni Maureen Godfrey (Njombe), Naba Magambo (Ruvuma), Happiness Samuel
(Kilimanjaro), Evelyan Baasa na Lilian Kamazima (Arusha).
Mariam Hussein (Open University), Maria Shilla na Camilla John (Dar India Ocean), Queen Latifa
Hashim na Doreen Beno (Miss Sinza), Sitti Mtemvu, (Chang'ombe), Salama Saleh na Neema Mollel (Miss Kurasini) kanda ya Temeke.
Warembo wengine ni Dorice Mollel (Singida), Rachel Clavery(Geita), Mary Emmanuel na Nicole Sarakikya (Shinyanga) na Doreen Robert.
Wengine ni Jihan Dimachk, Nasreen Abdul na Sabina Thomas, (Dar City Center),
Happiness Sosthenes (Ukonga), Naomi Kisaka (Dar city Center).
Taji la Redd's Miss Tanzania linashirikiliwa na Happiness Watimanywa kutoka kanda ya Mashariki.
Saturday, September 13, 2014
New
Miss Tanzania waingia kambini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment