Wastara asema Didas ni 'Iron lady' kama yeye - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 13, 2014

Wastara asema Didas ni 'Iron lady' kama yeye


Magendela Hamisi

MUIGIZAJI wa filamu, Wastara Juma amemshukuru, Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Seif kwa kufanikisha kupeleka wanasini nchini, Uingereza kutengeneza filamu.

Wastara akizungumza hivi karibuni katika uzinduzi wa filamu inayoitwa Mateso Yangu Ughaibuni alisema kuwa Watanzania wanaweza kupiga hatua ikiwa watatumia fursa hiyo vizuri.

Msanii huyo ni mhusika mkuu katika filamu hiyo iliyotengezwa nchini Uingereza na kushirikisha wasanii wa kitanzania na kuzinduliwa siku chache zilizopita katika viwanja vya Leaders Club.

Wasanii wengine walioshiriki filamu hiyo, Riyama Alli, Issa Mussa 'Cloud', Didas ambaye ndiye mtunzi wa hadithi hiyo na tayari ametoa ofa kwa wasanii wengine wenye filamu zao kuwasaidia kufanyia 'shooting' nchini Uingereza

.

No comments:

Post a Comment