MB Dog adondosha nyingine - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 13, 2014

MB Dog adondosha nyingine

Mwandishi Wetu

BAADA ya kufanya vema na wimbo unaitwa Mbona Umenuna, nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed 'MB Dog' (pichani) amesema kuwa kwa sasa amejipanga vizuri kuhakikisha anawapa raha mashabiki wake kwa kazi nzuri na zenye mvuto.

Aliongeza kuwa kwa sasa akiwa chini ya meneja wake mpya,  Joseph Mhonda ataachia kazi mpya ambayo itamweka katika mazingira mazuri ya kuleta ushindani katika soko la kizazi kipya kama alivyokuwa awali.

"Mashabiki wangu wasubiri kazi zangu mpya siku chache zijazo zikiambana na video kwa lengo la kuhakikisha mashabiki wanatapapata radha tofauti kwa wakati mmoja ili wapime uzito wa ujio wangu ambao naamini utaniweka pazuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini," alisema.

No comments:

Post a Comment