Magendela Hamisi
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ali Timbulo ametambulisha video ya wimbo wake inayoitwa Niende Zangu aliomshirikisha, Richard Mavoko 'Rich Mavoko'.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Timbulo ambaye alitambulika na wimbo unaoitwa Domo Langu ingawa kabla ya hapo alishaachia wimbo unaoitwa Ndoa japo haukumtambulisha vema alisema pia yuko katika mchakato kuachia kazi nyingine.
"Baada ya wiki mbili zijazo nitaachia kazi video ya wimbo wangu mpya unaoitwa Nakumisimis kutokana na wakati wowote kuanzia sasa nitaingia location kwa ajili ya maandalizi ya kazi hioyo ambayo inasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wangu," alisema.
No comments:
Post a Comment