Rais wa klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengele'Steve Nyerere' |
MUHESHIMU,Mthamini lakini usimwamini.... hayo ni maneno matatu ambayo yana maana kubwa katika jamii itazingatia katika kuendesha mfumo wa maisha.
Kwa maana katika jamii inashauriwa kuthaminiana na kuheshimiana ili kuhakikisha hatufanyiani matente mabaya ambayo yatasababisha amani kutoweka.
Binafsi nikiri kuwa watanzania siku zote wamelelewa katika maadili ya aina hiyo ndiyo maana pindi inapotokea matukio ya kinyama kila mtu, taasisi hujitokeza kulaani kwa maana si utamaduni uliojengwa na waasisi wa taifa hilo.
Ingawa watanzania wamejengewa misingi ya aina hiyo lakini si vema kujiweka huru na kumuamini kila unaoemuona usoni ukadhani ni mwema kwako.
Hivyo taadhari zinahitajika popote unapofanya shughuli zao hasa ukiwa katika sehemu za burudani ambako kuna mkusanyiko wa akila aina ya watu.
Ambao kila mmoja amelelewa katika mazingira yake, hivyo mtu unapokuwa katika mazingira ya burudani ambayo binafsi naamini ni hatari zaidi hasa unapokuwa unatumia kinywaji.
Katika hilo namaanisha kuwa unapokua kwenye kumbi unatumia kinywaji halafu ukanyanyuka kwenda msalani ni vema ukahakikisha unamaliza kinywaji chako au unyanyuka nacho ili kujihakikishia usalama zaidi.
Siku chache zilizopita nilikuwa katika moja ya shughuli ya kuwapata wanyange watakaoshiriki mashindano ya kumpata Miss Tanzania 2014.
Katika shughuli hiyo baadhi ya wasanii na wanamitindo wakubwa walikuwemo, kikubwa, kitu ambacho nilishangazwa ni kwa jinsi walivyokuwa hawana hadhari na vinywaji vyao.
Wasanii hao ambao wana majina hapa nchini walipoingia katika ukumbi waliagiza vinywaji na kuletewa juisi na hata kabla hawajamaliza walinyanyuka na kwenda kusikojulikana.
Ingawa niliamini ndiyo wametoka moja kwa moja lakini baada ya kama dakika 20 walirudi na kuketi na kuendelea na kunywa vinywaji vyao walivyoviacha.
Hakika hiyo ni hatari kubwa, tunashukuru kwamba waliofika katika shughuli hiyo inawezekana wengi wao walikuwa ni wastaarabu kwa kila mmoja kushika lake na kuendelea kutazama burudani ya iliyowakusanya hapo.
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa moja ya hoteli hapa jijini Dar es Salaam, na kunieleza kuwa ni kosa kubwa kunyanyuka na kuacha kunywaji bila kumwachia mtu unayemwamini.
Kwa maana kati ya ulionao hujui nani anachuki binfasi kwao hivyo anaweza kutumia nafasi ya kuacha kinywaji kufanya lolote analoweza kufanya na kukuweka katika mazingira hatarishi ikiwemo kupoteza uhai taratibu.
Kwa wasanii si kila uliyenaye anapenda mafanikio yako, nikirejea kwa wasanii hao baada ya kunyanyuka, walirejea baada ya dakika hizo na kuendelea kunywa kinywaji walichoacha, hakika jambo hilo lilinipa maswali mengi kichwani.
Je kama kungekuwa na mtu anataka kuwadhuru kwa kutumia vinywaji walivyoacha angeshindwa, je kama angefanikiwa matokeo yangekuaje, wasanii ebu chukueni taadhari na vinywaji vyenu.
Naamini neno ningejua mara zote huwa mwisho wakati tayari athari imeshakukuta, jihadharini kabla ya hatari kwa maana matitizo mengine yanaweza kudhuhirika ikiwa utachukua taadhari ya kumuani kila mtu kwa kuhisi ni mwema kwako.
Wapo baadhi ya wasanii waliodhurika aina hiyo, Mfano msanii na mpambani maarufu nchini Dotnata Poshi, kipindi fulani alidai kupata madhara ya kuwekewa sumu na mtu wake wa karibu.
Sababu ya kufanyiwa hivyo anazijua mwenyewe, kwa bahati nzuru aliwahi kupata tiba iliyosaidia kunusuru maisha yake kama asingewahi kupata matibabu pengine leo tusingekuwa na msani huyo ambaye pia ni mdau wa masumbwi.
Wakati mwingine msanii anapojikuta na madhara hayo uhisi amerogwa kumbe ni 'slow poison' ndiyo inayomaliza iliyokana tokana na kushindwa kujilinda vinywaji vyao wanapokuwa na kundi kubwa watu.
pindi wanapokuwa na starehe zao na kufanya wabaya wao kutumia
Hivyo wanapokuwa katika starehe wanatakiwa kutomuamini kila anayemuona machoni mwake kwa maana wengine mioyo yao haiko safi na kikulacho kinguoni mwako.
Wapasawa kuhakikisha wanapokuwa wanatumia vinywaji kabla ya kuondoka wavimalize ili wanaporejea waanze upya kutumia glasi na kinywaji kwa lengo la kujilinda na maadui ambao wanaweza kutumia nafasi hiyo kudhuru.
Binafsi naamini nimeeleweka vizuri katika hilo, wasanii wajihadhari na watu wanaoweza kutumia nafasi ya kuwadhuru kwa vinywaji walivyoviacha na kukirejea tena, ukidhani uko salama kumbe tayari umeshaumizwa.
Hivyo narejea awali kuwa kinachotakiwa ni kuwaheshimu ulionao, uwathamini lakini si vema ukawaamini kwa asilimia zote kwani lolote wanaweza kufanya kwa ajili tu ya chuki binfasi kutokana na mafanikio ulionayo au la.
magendela@gmail.com
No comments:
Post a Comment