Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni
mwa nchi chache barani Afrika ambazo zinatekeleza dhana ya
ushirikishwaji wa Jamii katika uhifadhi wa kivitendo kwa kutoa fursa kwa
wananchi kushiriki moja kwa moja katika kusimamia rasilimali za
wanyamapori
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu wa Maliasili na
Utalii, Juma Mkomi wakati akifungua warsha ya kupitia na kuthibitisha
mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya
Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha
Amesisitiza
kuwa WMAs ni kinga (buffer) muhimu kwa maeneo ya Hifadhi za Taifa,
Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Ngorongoro na Mapori Tengefu.
Mkomi
amesema bila WMAs changamoto za kiuhifadhi zitaathiri moja kwa moja
Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Hifadhi ya Ngorongoro na Mapori
Tengefu
Kutokana na umuhimu huo, Mkomi ametoa wito kwa Wadau wa
Uhifadhi nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za
kuendeleza WMAs ili kuziwezesha kujisimamia na kujiendesha.
Ameongeza
kuwa kupitia ushirikishwaji huo Jamii zimekuwa zikinufaika na matunda
yatokanayo na shughuli za uhifadhi katika maeneo yao kwa kujiletea
maendeleo na huduma za kijamii ikiwemo shule na zahanati
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha
amesema toka kuanzishwa kwa dhana ya WMAs jamii imekuwa ikishiriki
kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori hali
inayopelekea ulinzi wa kuwa madhubuti
Amesema kufuatia hali hiyo
maeneo ya WMAs yamekuwa ya kuvutia shughuli mbalimbali za uwekezaji kwa
ajili ya utalii wa picha, uwindaji wa kitalii na uwekezaji kwa ajili ya
hewa ya ukaa
Akizungumzia manufaa ya ushirikishwaji huo, Dkt.
Msuha amesema katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2021 jumla ya jumuiya
15 zenya mikataba ya uwekezaji katika uwindaji wa kitalii zimeweza
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 4.91 ambazo zimewezesha utekelezaji
wa miradi ya maendeleo ikiwemo ufadhili wa wanafunzi kusoma katika vyuo
vikuuNaibu
Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akizungumza wakati akifungua
warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa
maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo
Jijini Arusha
Mkurugenzi
wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha akizungumza kabla ya kumkaribisha
aibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi kwa ajili kufungua warsha
ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo
ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini
Arusha
Naibu
Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi (kulia) akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori
nchini John Salehe wakati wa hafla ya kufungua warsha ya kupitia na
kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za
Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini Arusha
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi UNDP, Gertrude Lyatuu akizungumza wakati wa hafla
ya kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na
uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs)
iliyofanyika leo Jijini Arusha ambapo amewataka Wadau hao kuwa mstari wa
mbele katika kulinda maeneo ya Hifadhi
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori nchini John
Salehe akizungumza mbele ya Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma
Mkomi (kulia) ambapo ameushukuru Uongozi wa Wizara wa Maliasili na
Utalii kwa kuendelea changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiikumba
Jumuiya za Wanyamapori nchini
Naibu
Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja
na Wenyeviti wa Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) mara baada ya
kufungua warsha ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na
uendeshaji wa maeneo ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs)
iliyofanyika leo Jijini Arusha
Naibu
Katibu wa Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akiwa kwenye picha ya pamoja
na Wajumbe wa Sekretariet ya maandalizi mara baada ya kufungua warsha
ya kupitia na kuthibitisha mkakati wa usimamizi na uendeshaji wa maeneo
ya Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) iliyofanyika leo Jijini
Arusha
Friday, September 23, 2022
New
TANZANIA YATAJWA KUWA NI MIONGONI MWA NCHI CHACHE BARANI AFRIKA KATIKA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KWENYE UHIFADHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment