Huduma
za kibingwa za Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) zimeanza
kutolewa katika hospitali mpya na ya kisasa ya rufaa ya kanda kusini
Mtwara ambapo kwa mara ya kwanza historia imeandikwa kwa mgonjwa wa
kwanza kufanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.
Upasuaji huo wa
kibingwa wa Mifupa umefanywa na jopo la madaktari bingwa ,wauguzi na
wataalam wa usingizi kutoka MOI kwa kushirikiana na wataalamu wa
hospitali ya Rufaa ya Kusini Mtwara.
Kiongozi wa jopo la
wataalamu kutoka MOI, Dkt. Albert Ulimali amesema jopo la wataalam 11
limepiga kambi ya siku tano katika hospitali ya kanda Mtwara kwaajili ya
kutoka huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya
fahamu ikiwa ni pamoja na kuwafanyia upasuaji wagonjwa.
“Tuko
hapa katika hospitali ya kanda kusini, tumetumwa na kiongozi wetu wa MOI
Dkt. Respicious Boniface tuje kuanzisha huduma zetu hapa, tunashukuru
muitikio wa wananchi umekua mkubwa ambapo kwa siku ya kwanza peke yake
tuliwahudumia zaidi ya wagonjwa ya 280” Alisema Dkt. Ulimali
Dkt.
Ulimali amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia
Suluhu Hassan kwa ujenzi wa hospitali kanda kusini pamoja na usimikaji
wa vifaa vya kisasa. Pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmad
Abass pamoja na Mkuu wa Wilaya Mtwara Mh Dunstan Kyoba kwa mapokezi
mazuri.
Daktari bingwa wa Mifupa kutoka MOI, Dkt Tumaini Minja
amesema upasuaji wa kwanza katika hospitali hiyo umefanyika kwa
mafanikio makubwa na huduma hizo zitaendelea kupatikana hospitalini hapo
hivyo wakazi wa mikoa ya kusini wajitokeze kupata huduma.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kusini Mtwara Dkt Jeofrey
Ngomo ameishukuru Taasisi ya MOI kwa kusogeza huduma za kibingwa kwa
wakazi wa mikoa ya kusini ambapo waogonjwa hawatalazimika kufuata huduma
hizo Dar es Salaam.
.jpeg)

.jpeg)





No comments:
Post a Comment