MKUU
wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kulia akikagua gwaride la vijana
wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni Jenerali Venance
Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani Handeni Mkoani Tanga
Gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni
Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani
Handeni Mkoani Tanga wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Omari Mgumba wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
gwaride la vijana wahitimu wa mafunzo kwa mujibu wa sheria Operesheni
Jenerali Venance Mabeyo kikosi cha 835 KJ cha Mgambo JKT wilayani
Handeni Mkoani Tanga wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
Na Oscar Assenga HANDENI.
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka vijana waliohitimu wa mafunzo
ya Operesheni Mabeyo 2022 wanakwenda kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini
kuhakikisha wanatumia vizuri mitandao ya kijamii kwa faida ikiwemo
kujjiepusha na matumizi mabaya.
na sio vyenginevyo
RC
Mgumba aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya katika kambi ya JKT
Kabuku 835 KJ wilayani Handeni wa mujibu wa Sheria Operesheni Jenerali
Venance Mabeyo 2022,ambapo alisema kwa sababu vijana wengine waliopo
vyuoni wamekuwa na uhuru uliopitiliza na kufanya mambo bila uwepo wa
usimamizi.
Alisema lazima wazazi washirikiane katika kuwatembelea
watoto wao mara kwa mara kwa maana unaweza kujua mtoto wao anasoma
kumbe anasomeshwa jambo ambalo baadae linaweza kuwa na athari kwake na
Jamii kwa ujumla.
"Niwasihi wazazi wenzangu muwe mnafanya
kuwatembelea watoto wenu wanapokuwa vyuoni lakini wahitumu leo niwaase
mkatumie vizuri mitandao ya kijamii kwa ajili ya faida na sio
nyenginevyo maana vijana wengine waliopo vyuoni anaweza kudanganywa
mwenye mitandao ya kijamii ukashurutishwa jambo ambalo unaweza kufanya
kwa tamaa"Alisema
Mkuu huyo wa Mkoa alisema matokeo yake
wanadhalilisha wazee wao Jamii na Ndugu na Taifa kwa ujumla hivyo
hakikisheni suala la nidhamu wanalishikilia kweli hasa wale wanaoenda
kuishi vyuoni.
"Kwa sababu mtakumbana na watu mbalimbali ikiwemo
wanasheria wasije kuwapotosha nyie mmeiva na mmefundwa nidhami na
uadilifu kaishini maisha hayo"Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Awali
akizungumza wakati wa ufunguji wa mafunzo hayo Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele aliwataka wahitimu wa
mafunzo wasiende kutu mika vibaya katika maeneo mrakayokuwepo wakati
wote mkumbuke kiapo mlichoapa.
Alisema kuwa kama wanavyofahamu
majukumu ya JKT ni malezi ya vijana na uzalishaji wa mali na kufanya
shughuli za ulinzi wa Taifa katika kutekeleza majukumu hayo ya kila
siku.
Hata hivyo alisema hivyo kutolewa mafunzo hayo kwa vijana
wa mujibu wa sheria na mafunzo ya mujibu wa sheria op Jenarali Mabeyo
yamekuchukua muda wa majuma 12 mfululizo.
Mkuu wa Jkt alisema
kwamba wahitimu hao wamejifunzamasomo mbalimbi yakiwemo ya uzalishaji
mali,nadharia na vitendo kwa ujumla lengo kukuza moyo wa uzalendo
kuwajengea nidhamu ,ukakamavu na ujasiri.
Alisema hiyo itawafanya wajitambue kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuilinda,kuijenga na kuitetea nchi yao.
Naye
kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha 835 KJ JKT Kabuku Luteni Kanali
Raymond Mwanri alisema vijana hao wakiwa kwenye mafunzo hayo wamejifunza
mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi wa Taifa lao,Uzalendo na utii kwa
mamlaka zilizowekwa kwa mujibu wa sheria .
Hata hivyo aliwataka
wahitimu hao kuhakikisha wanakiishi kiapo hicho huku akieleza wamefaulu
katika viwango mbalimbali vya kuhitimua mafunzo hayo.
Hata hivyo
kwa upande Mkuu wa Mafunzo wa JKT Tanzania Kanali Aisha Matanza alisema
mafunzo ya vijana ya kujitolea kwa mujibu wa sheria ya Jenero Mabeyo
yamekuwa chachu kuweza kuwaimarisha vijana kuwafanya wakakamavu na
wazalendo kwa nchi yao.
Wednesday, September 28, 2022
New
RC MGUMBA AWATAKA WAHITIMU WA MAFUNZO OPERESHENI MABEYO 2022 KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA TIJA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment