Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Mary Masanja amefungua warsha ya siku mbili ya wadau wa
uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa
uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya
kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini.
Warsha hiyo imefunguliwa Septemba 27,2022 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika ufunguzi huo, Mhe. Masanja amesema misitu ya mikoko na majani ya
baharini inatarajiwa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa bluu kwa
kuhifadhi hewa ya ukaa mara tano zaidi ya misitu ya kawaida.
Ameelekeza
washiriki wa warsha hiyo kuibua masuala muhimu yatakayoisaidia Serikali
kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya biashara ya hewa ya ukaa.
Ametaja
faida nyingine za misitu ya mikoko kuwa ni kusaidia kukabiliana na
athari za kimazingira kama mabadiliko ya tabia ya nchi, mmomonyoko wa
udongo na vimbunga baharini, kusaidia uwepo wa mazalia ya samaki, chanzo
cha kuni, mbao na milunda ya kujengea.
Aidha, amesema uwepo wa
shughuli za kibinadamu katika misitu ya mikoko, hupelekea kupotea kwa
mikoko na kuathiri ukuaji wa uchumi wa bluu.
Mhe. Masanja
amefafanua kuwa ili kukabiliana na changamoto za upotevu wa misitu ya
mikoko Serikali itatoa elimu kwa wananchi namna bora ya kutunza mikoko
hiyo na kushiriki moja kwa moja katika uhifadhi wa mikoko kwa
kushirikiana na sekta binafsi.
Naye, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala
wa Huduma za Misitu za Misitu Tanzania, Prof Dos Santos Silayo amesema
wananchi wanatakiwa wawe na mifumo endelevu ya kupata kipato
itakayowawezesha kukidhi mahitaji yao bila kukata mikoko.
“Mifumo
hii itawawezesha wananchi kuvuna hewa ya ukaa na kujipatia fedha bila
kuathiri mikoko kwa mfano kufanya shughuli za ufugaji nyuki na utalii”
amefafanua Prof. Silayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uvuvi,
Wizara ya Uchumi wa Bluu Zanzibar, Dkt. Salumu Hemedi amesema kuna
uhusiano mkubwa wa uchumi wa bluu na biashara ya hewa ya ukaa.
Amesema
biashara ya hewa ya ukaa inafanyika sana katika mataifa mengi duniani
ambayo yana viwanda yanatumia hewa ya ukaa katika nchi ambazo zina
misitu ambazo zinalipwa ili kutunza misitu.
Warsha hiyo
imehudhuriwa wa Maafisa kutoka Serikali ya Tanzania na Kenya,
Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Wadau wa Uhifadhiwa Mifumo Ikolojia ya
Bluu pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul (kushoto) wakikata utepe kama ishara ya kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul akizungumza katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii,Deusdedit Bwoyo akitoa maneno ya utangulizi katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumzia namna taasisi yake inavyoshiriki katika utunzaji wa misitu ya mikoko katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati)katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment