Na mwandishi wa NCAA, Arusha.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) leo tarehe 28
Septemba, 2022 amezindua bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro ambayo iliteuliwa hivi karibuni.
Katika tukio hilo
Mhe. Waziri Chana ameielekeza Bodi hiyo kutekeleza mkakati wa serikali
wa kuboresha miundimbinu ya utalii, kuimarisha shughuli za Uhifadhi na
kuongeza jitihada za kuongeza idadi ya watalii nchini kufikia watalii
milioni 5 mwaka 2025.
Pia ameielekeza Bodi hiyo kwa kushirikiana
na menejimenti ya NCAA kuendelea kubuni mazao mapya ya utalii ili
kuvutia wageni wanaotembelea Nchi yetu pamoja na kupanga mikakati ya
kutangaza na kukuza utalii wa vivutio vilivyoko Ngorongoro.
“Sambamba
na kuboresha miundombinu ya Utalii pia tuendelee kuhifadhi, kulinda
maliasili lakini kubuni mazao mapya ya utalii yatakayosaidia idadi ya
wageni kuongezeka kufikia idadi ya milioni 5 mwaka 2025 kama
tunavyoelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi” Mhe. Balozi Dkt. Pindi
Chana Waziri wa Maliasili na Utalii.
Mwenyekiti wa bodi ya
Wakurugenzi NCAA Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo ameeleza kuwa Bodi
anayoiongoza imejipanga kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kusimamia
shughuli za Uhifadhi, Utalii, Maendeleo ya jamii ili kuhakikisha kuwa
rasilimali za nchi zinahifadhiwa, kutunzwa na kuongeza tija ili ziwe na
manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Tumeona jitihada
mbalimbali za serikali kutangaza utalii hasa kupitia kampeni ya Mhe.
Rais ya Tanzania The Royal Tour na kupelekea kuongezeka kwa idadi ya
watalii nchini hasa baada ya janga la UVIKO-19 lililotikisa dunia.
"Bodi
ya Wakurugenzi tunaahidi kuendeleza jitihada hizi kuhakikisha tunafikia
idadi ya watalii milioni tano (5) kwa mwaka 2025 kama malengo ya Wizara
yanavyosema” Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi, NCAA.
Jenerali Mstaafu Mabeyo ameongeza kuwa Bodi
anayoiongoza itahakikisha Mamlaka inabuni mazao mapya ya utalii,
kuboresha huduma kwa watalii na kutumia mikakati madhubuti ya kutangaza
vivutio ili kuvutia wageni wengi zaidi na kuongeza mapato kwa nchi.
Naibu
Katibu Mkuu - Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Juma Mkomi ameeleza
kuwa kutokana na jitihada na mikakati mbalimbali ya serikali ya
kutangaza utalii hasa kupitia kampeni ya Mhe. Rais ya Tanzania, The
Royal Tour idadi ya wageni imeendelea kuongezeka na kufikia 425,386 na
mapato kuongezeka na kufikia TZS. Bilioni 91.1 mwaka 2021/22.
Amefafanua
kuwa Serikali inaamini idadi hii ya watalii na mapato yataongezeka
maradufu kwa mwaka 2022/23 kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa
na Serikali.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt.
Freddy Manongi, Hifadhi ya Ngorongoro ni eneo pekee Afrika lenye hadhi
tatu kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni Duniani (UNESCO).
Amezitaja
hadhi hizo kuwa ni Hadhi hizo ni pamoja na Eneo la Urithi wa Dunia
Mchanganyiko (Mixed World Heritage Site), Eneo la Hifadhi Bayoanuai (Man
and Biosphere Reserve) na Eneo la Utalii wa Jiolojia (UNESCO Global
Geopark), Kutokana na hadhi hizi za kimataifa, eneo hili limekua
likivutia wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani ambao huchangia
mapato makubwa kwa serikali na wananchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akikata
utepe wa Nyaraka za Sheria mbalimbali kama kitendea kazi kwa ajili ya
kumkabidhi Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Mstaafu
Venance Mabeyo leo Septemba 28,2022 jijini Arusha wakati akizindua bodi
ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliyoteuliwa hivi
karibuni,kulia anaeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Mary Masanja
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akimkabidhi Nyaraka
za Sheria mbalimbali kama kitendea kazi Mwenyekiti wa bodi ya
Wakurugenzi wa NCAA Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo leo Septemba 28,2022
jijini Arusha wakati akizindua bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo
iliyoteuliwa hivi karibuni
Mwenyekiti
wa bodi ya Wakurugenzi wa NCAA Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo
akizungumza jambo mbele ya Wageni waalikwa wa hafla hiyo leo Septemba
28,2022 jijini Arusha mara baada ya kuzinduliwa bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni
Wednesday, September 28, 2022
New
Balozi Dkt . Chana azindua Bodi ya Wakurugenzi NCAA .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment