-MBUNGE HHAYUMA AFAGILIA ZIARA YA WAZIRI WA TAMISEMI HANANG'
Na Mwandishi wetu, Hanang'
MBUNGE
wa Jimbo la Hanang' Mkoani Manyara, mhandisi Samwel Hhayuma Xaday
amesema ziara ya siku moja ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa kwenye jimbo
lake imeleta mafanikio makubwa.
Mhandisi Hhayuma akizungumza baada ya ziara hiyo amesema imeleta mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya na miundombinu.
Amesema
wamepata nyongeza ya kilomita moja ya lami kwenye mji wa Katesh, hivyo
mwaka wa fedha wa 22/23 zitajengwa kilomita mbili za lami.
"Ujenzi
wa stendi mpya ya kisasa ya sh5.6 bilioni unaendelea, tumepata gari
mbili za wagonjwa na nyongeza ya fedha ya kukarabati barabara ya
Setchet-Hirbadaw- Zinga baada ya tathimini kufanyika," amesema mhandisi
Hhayuma.
Amesema pia utafanyika ujenzi wa barabara ya Waama-Diloda-Mureru kwa 33 kilomita 33 kwa mwaka huu wa fedha.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amesema ziara hiyo ya
siku mbili ya Waziri Bashungwa imeendelea kwenye wilayani Mbulu.
Makongoro
amesema akiwa wilayani Mbulu, Waziri Bashungwa atakagua miradi ya
maendeleo ya sekta ya elimu, afya, barabara na utawala kwenye
Halmashauri mbili.
Amesema katika ziara hiyo Waziri Bashungwa ameambatana na Kaimu Katibu Mkuu Tamisemi Dk Charles Msonde.
No comments:
Post a Comment