Na WAF- KAGERA.
Katibu
mkuu Wizara Prof. Abel Makubi ameelekeza Wataalamu wa afya katika mipaka
kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola ili
kuweza kuutambua na kuuzuia endapo utaingia nchini.
Prof. Makubi
ametoa rai hiyo, mapema leo wakati akitembelea Mpaka wa Tanzania na
Uganda -MTUKULA na kukagua zoezi la uchunguzi wa abiria wanaoingia
nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo aliyoambatana na Mkuu wa
Wilaya ya Misenyi, Prof. Makubi ameshuhudia upimaji wa kutumia
Thermoscans ikiwa ni moja ya njia ya kutambua hali ya maambukizi endapo
mgonjwa atatokea.
Hata hivyo, Prof. Makubi ameelekeza kutumika
kwa dodoso la kutambua dalili za ugonjwa wa Ebola kama njia nyingine ya
kutambua hali ya maambukizi endapo mgonjwa atatokea.
Kwa upande
mwingine, Prof. Makubi amekutana na wakazi wa mpakani katika eneo la
Mtukura, huku akielekeza Wataalamu wa Afya kutoa elimu kwa wakazi hao
juu ya namna bora ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili usiingie
nchini.
Aidha, Prof. Makubi ameendelea kuhimiza kuwekwa kwa
mifumo ya kunawa mikono katika mitaa, maeneo ya vituo vya abiria,
daladala, sehemu za ibada, ofisi na majumbani ikiwa ni sehemu ya
mikakati ya kupambana dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa
Ebola.

No comments:
Post a Comment