NA SAID MWISHEHE
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
imesema kuna mkakati wa kampeni ya kitaifa itakaofanyika nchi nzima
kutoa elimu mtandao kwa wananchi ili kuhakikisha sheria,kanuni na
miongozo iliyopo inafuatwa kwa lengo la kuepuka changamoto
zinazojitokeza kutokana na matumizi ya mitandao.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa vijana wa kujadili
Usimamizi wa masuala ya mitandao uliondaliwa na Shirika la Intanet
Society Tanzania(IST), Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya usalama mitandao
Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Stephen
Wangwe amesema kampeni hiyo inatarajia kuanza rasmi Oktoba mwaka huu.
“Pamoja
na mambo mengine lakini kwa ngazi ya Wizara tunahusika zaidi na
utengenezaji wa sera, sheria miongozo na taratibu mbalimbali za
kutusaidia na kuwasaidia wananchi kuwa na matumizi salama ya mitandao
yetu , hivyo siku ya leo miongoni mwa mambo niliyowasilisha kwa vijana
hawa nimewaeleza Septemba 23 kwenye Bunge letu ule muswada wa Sheria ya
Ulinzi wa taarifa binafsi umesomwa rasmi na sasa ni nyaraka ya umma.
“Kwa
hiyo watu ambao hawakupata fursa tangu mchakato umeanza huu ndio muda
wao wa kupitia na kuaingalia wanaweza kutoa maoni gani na yote ni
kuhakikisha tunakuwa na Sheria itakayokuwa nzuri kwa sisi wote.Pia ni
wakati mzuri kwa umma kutafuta muda na wakati kuielewa hii sheria na
kujua ni mambo gani ya kwenda kushughulikia,”amesema.
Ameongeza
kuwa uwepo wa Sheria hiyo itakwenda kufungua fursa kwani kuna baadhi ya
wawekezaji wakubwa wanaoshughulika na masuala ya TEHAMA wanabanwa na
nchi zao kuja kuwekeza kwenye nchi ambazo hazina mfumo wa kisheria wa
ulinzi wa taarifa binafsi.Hivyo ujio wa sheria ni matarajio ya Serikali
wawekezaji wakubwa kutoka nchi mbalimbali watakuja kuwekeza nchini
kwenye masuala ya mtandao.
“Lingine
ambalo nimesisitiza ni kwamba katika masuala ya usalama wa mtandao ni
muhimu kupata uelewa yaani elimu kwa umma kwani watu wengi huwa
wanapata matatizo kwasababu uelewa wao, inawezakana hayupo vizuri katika
maeneo fulani fulani hususan wanaweza kupata madahara fulani anapofanya
jambo fulani kwenye mtandao.
“Unakuta watu wanafanya jambo
fulani kwa faragha au starehe zao lakini baadae inawaletea matatizo.
Hivyo Serikali tunao mkakati wa kitaifa wa kutoa elimu kwa umma kuhusu
elimu mtandao na tutazunguka katika makundi yote kuanzia ngazi za
Serikali na binafsi, makundi ya wanafunzi, kaya mbalimbali na
kuhakikisha makundi yote ya umma yanafikiwa na kuelimishwa namna gani ya
kuweza kutumia mitandao vizuri ili isituletee changamoto katika siku za
usoni,”amesema Mhandisi Wangwe.
Amesisitiza kampeni itaanza
Oktoba mwaka huu kwa kuwa mwezi huo ndio mwezi wa usalama katika mtandao
duniani, hivyo wameona ndio utakuwa wakati muafaka wa sisi kuanza
kampeni hiyo rasmi.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Intanet
Tanzania ambaye pia ni Mratibu wa Jukwaa la Usimamizi wa Mitandao
nchini Nazar Kilama amesema mkutano wa usimamizi wa masuala ya mitandao
kwa upande wa vijana unalenga kuwajengea vijana uwezo wa kushiriki
katika mifumo ya Intanet au mifumo ya masuala ya mitandao duniani.
“Hii
mikutano imekuwa ikifanyika katika kila nchi, kikanda , Afrika na
Dunia, kwa upande wa Tanzania ndio inaitwa foramu ya Tanzania , upande
wa Afrika Mashariki inaitwa foramu ya Afrika Mashariki, Afrika na dunia
ambayo iko chini ya umoja wa mataifa.Kwa hiyo lengo la hii foramu kwanza
ni kuendelea kuwajengea vijana uwezo wa namna ya kushiriki hii mikutano
ya kitaifa, kikanda na kidunia kwenye masuala ya usimamizi wa mtandao.
“Kwa
hiyo hii foramu ya kwetu hapa kwanza ni kuwapa vijana uwezo wa kuweza
kushiriki kwenye mijadala mbalimbali ambayo inafanyika kwenye hayo
maeneo mengine ambayo nimeyataja mkapa kuelekea huko umoja wa mataifa,
tunaamini vijana wana uwezo mkubwa tu wa kushiriki lakini inahitaji pia
watu wanaojua kama sisi na wengine ambao wako kwenye hii mifumo ya
Tehama kutoa muda wao ili kuwajengea uwezo vijana na kushiriki vizuri
kama Tanzania kwenye hayo maeneo mengine.
“Leo tumekuwa na
mkutano wa pili , mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 2021 na huu ni
mkutano wa pili na mwakani tutaendelea kuwajengea vijana uwezo maana
watakuwepo tu na wenye uwezo tungependa waendelee kuwajengea vijana
uwezo.Pia tunawashukuru Wizara kuja kutuunga mkono,”amesema.
Wakati
huo huo Mwenyekiti wa Foramu hiyo Catherine Fungo amesema mkutano huo
umeshirikisha vijana 50 ambao wamepatkana baada ya kujaza fomu na wengi
ni wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali.“Lengo vijana kujengewa uwezo
ambao utawawezesha kuzungumza na kutoa maoni na ushauri kabla ya maamuzi
kufanyika.”
Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Shephen Wangwe ( wa kwanza kushoto) akifuatilia majadiliano wakati wa mkutano wa vijana unaohusu masuala ya Mtandao.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye Mkutano wa Vijana wenye lengo la kujengewa uwezo kuhusu masuala ya Mtandao.Mmoja ya washiriki akitoa maoni yake kuhusu matumizi sahihi ya masuala ya Mtandao kwa vijana
No comments:
Post a Comment