Na Imma Msumba ; Arusha
Wasindikaji
wa vyakula pamoja na Wafanyabiashara wametakiwa kuwa na utaratibu
unaoonesha mchanganyiko unaotumika katika bidhaa zao ili kumruhusu mlaji
kufanya maamuzi kabla yakufanya manunuzi nakujiepusha na magonjwa
yasiyo ambukiza yanayotokana na baadhi ya vyakula.
Mtaalamu wa
Afya na Mazoezi kutoka shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyo ambukiza,
Dkt. Waziri Ndonde akizungumza jijiji Arusha wakati wa majadiliako
yakufikisha elimu kwa jamii namna yakujiepusha na tabia bwete na ulaji
wa vyakula usiozingatia viwango, ambaye amesema watu wengi hununua
vyakula bila kuzingatia mchanganyiko uliopo nakupata athari.
Dkt.
Ndonde amesema kuwa kwa sasa Wanafanya tafiti zitakazosaidia kuondokana
na kasi ya kuenea kwa magonjwa yasiyo ambuliza yanayo sababishwa na
matumizi ya vyakula visivyo faa.
Pia Dkt Ndonde, ameongeza kuwa
namna pekee itakayo saidia kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo
kisukari pamoja na magonjwa ya moyo ni pamoja na kuacha tabia bwete na
kuanza kufanya mazoezi ikiwa ni njia pekee ya kupunguza athari
zitokanazo na matumizi ya vyakula.
Hata hivyo Dkt Ndonde amesema
ipo haja ya mamlaka zinazo simamia chakula na dawa kutunga sheria
madhubiti pamoja na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyakula na
dawa ikiwa ni mpango wa kusaidia Afya ya jamii.
Thursday, September 29, 2022
New
WASINDIKAJI WA VYAKULA WATAKIWA KUWEKA WAZI USINDIKAJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment