Na Mwandishi wetu, Babati
MKOA wa Manyara umepata viongozi wapya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya sita za Mkoa huo.
Katibu
wa UVCCM Mkoa wa Manyara, Ibrahim Kandumila akizungumza mjini Babati
amesema uchaguzi huo umekamilika kwa asilimia 100 na kufanyika kwa
amani.
Amewataja
wenyeviti hao waliochaguliwa na wilaya zao kwenye mabano ni Solomon
Mekiory (Babati vijijini), Justin Ammi (Hanang') na Magdalena Urono
(Babati mjini).
Amewataja wengine ni Hamza Mngia (Kiteto), Timothy Mollel (Simanjiro) na Elisante Michael (Mbulu).
"Nawapongeza
na kuwashukuru wote walioshinda ila watimize majukumu yao ipasavyo na
ambao kura hazikitosha wawape ushirikiano wale walioshinda," amesema
Kandumila.
Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya ya Babati Vijijini Solomon Melkiory amewashukuru
wajumbe wa jumuiya hiyo kwa kumchagua ili awaongoze na ameomba
ushirikiano kwao.
Mwandishi
wa kituo cha FM Manyara na AYO TV, Charles Mangwe ambaye ni mjumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Babati Vijijini kupitia UVCCM
amewashukuru wajumbe kwa kumpa kura za ushindi.
Mjumbe
wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Babati mjini kupitia UVCCM Husna
Mdinku ameomba ushirikiano kwa wajumbe hao na kuahidi kuwaunganisha
kupitia nafasi hiyo.
Mjumbe
wa mkutano mkuu wa UVCCM Wilaya ya Babati mjini Elias Ernest ambaye ni
mwandishi wa kituo cha Wasafi amewashukuru wajumbe kwa kumpatia nafasi
hiyo.
No comments:
Post a Comment