Na. OMM Rukwa
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amesema atahakikisha fedha zote
zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya 191
kwenye shule za sekondari mkoani humo zinatumika kama ilivyokusudiwa ili
wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 waweze kuanza masomo yao kwa
wakati.
Serikali
ya Awamu ya Sita imeupatia mkoa wa Rukwa shilingi Bilioni Tatu na
Milioni Mia Nane na Elfu Ishirini (3,820,000,000/-) kwa ajili ya ujenzi
wa vyumba vipya vya madarasa katika halmashauri nne za mkoa wa Rukwa
ambapo kila darasa litajengwa kwa shilingi Milioni Ishirini kupitia
mfumo wa “Force Account”.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo (03 Oktoba,2023) ofisini kwake mjini
Sumbawanga Mhe. Sendiga alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha
wanafunzi wote wanapata mahala bora na salama kusomea.
“Natoa
wito kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kufuatilia kwa ukaribu ujenzi
wa madarasa hayo ili yaweze kukamilika kwa muda yaani ndani ya siku
Sabini na Tano (75) kama alivyoelekeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -
TAMISEMI na kwa ubora ulioelekezwa pamoja na kukamilisha utengenezaji wa
madawati yake” alisisitiza Sendiga.
Katika
taarifa yake, Mhe. Sendiga alisema mkoa umefanya maoteo ya Wanafunzi
26,655 wa kujiunga Kidato cha kwanza mwezi Januari, 2023. Maoteo hayo
ni kutoka jumla ya watahiniwa 33,319 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa
Kumaliza Elimu ya msingi mwaka 2022 sawa na asilimia 80 ya ufaulu ambapo
wanafunzi hao watahitaji jumla ya madarasa 534 ambapo madarasa yaliyopo
ni 343 na upungufu ni madarasa 191.
Sendiga
alitaja mchanganuo wa idadi ya vyumba 191 vya madarasa kwa kila
Halmashauri kwenye mabano, Manispaa ya Sumbawanga (56) sawa na
shilingi 1,120,000,000/= ,Halmashauri ya Nkasi (26) sawa na shilingi
520,000,000/= Halmashauri ya Sumbawanga (46) sawa na shilingi
920,000,000/= na Halmashauri ya Kalambo (63) sawa na shilingi
1,260,000,000/=.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu mapokezi ya shilingi Bilioni 3.8 zitakazojenga vyumba vipya 191
vya madarasa kwenye halmashauri nne za Rukwa halfa ilyofanyika leo mjini
Sumbawanga.
No comments:
Post a Comment