Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George
Simbachawene akizungumza na Wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Wazee Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022.
Na WMJJWM, Dodoma
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
ameziagiza mamlaka za Serikali za Mitaa kuwashirikisha Wazee kupitia
mabaraza yao kushiriki kwenye vikao vya maamuzi kuanzia ngazi za vijiji
na mitaa hadi Mabaraza ya Madiwani.
Akizungumza
kwa niaba ya Mhe. Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati wa maadhimisho ya
Kitaifa ya Siku ya Wazee yaliyofanyika Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022.
Mhe.
Majaliwa amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali kwa lengo la
kuhakikisha Jamii inawatambua na kuwathamini wazee ikiwemo kuanzisha
Kampeni ya mpishe Mzee kwenye maeneo mbalimbali ya kutolea Huduma.
"Kila
Halmashauri iweke maeneo mazuri ya kukaa wakati wa mikutano ya mabaraza
ya Madiwani na Wazee wanapo jadili mambo yao mzingatie Uzalendo na
ujenzi wa maadili mema kwa watoto wetu" amesema Simbachawene
Simbachawene
amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua Makundi muhimu
hususani Wazee kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya kushughulikia Makundi hayo kwani
kabla
Makundi hayo yalikuwa ,yanakosa mahali maalum pa kupeleka Masuala yao .
Ameongeza
kwamba, Serikali inaendelea kuelimisha jamii kuzingatia ulinzi na
usalama kwa Wazee Kwa kuanzisha mabaraza ya wazee 20749 Kwa lengo la
kuwapa fursa ya kujadili mambo yao na kuwa chombo cha kushauri Jamii.
Waziri
Simbachawene ametumia nafasi hiyo kutoa Rai kwa viongozi na Wazee kuwa
pamoja na kutumia mabaraza hayo kujadili Ustawi wao wahakikisha umoja na
Jumuiya nyingine za Wazee zinatambuliwa na kusajiliwa katika maeneo yao
na taarifa za utekelezaji wa mabaraza ya Wazee zijumuishwe kwenye
kamati za Maendeleo ili mawazo yao yaweze kuzingatiwa na kufanyiwa kazi.
Ametoa wito kwa Jamii kushirikiana kuzuia ukatili kuliko kunyamaza na hatimaye kunung'unuka na kuombolea matukio yanapotokea.
Kwa
upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi
Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema maadhimisho hayo ni matokeo ya
maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kuanzisha Wizara hii.
"Uzinduzi wa Baraza la Taifa la Wazee ni ishara ya Serikali kuwathamini Wazee kupitia mabaraza yao
Akizungumza
katika Maadhimisho hayo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.
Grace Magembe amebainisha kuwa, TAMISEMI imeendelea na zoezi la
kuwatambua wazee na hadi sasa imetambua 2117637 kutoka Mikoa yote 26
bapo wanaume ni 1382468 na wanawake 735169.
"Tumetoa
Bima ya Afya ya Jamii kwa Wazee ili wapate huduma kwenye vituo vya Afya
ngazi ya msingi kuanzia zahanati Hadi hospitali za Wilaya" amesema Dkt.
Grace.
Dkt.
Grace ameongeza kuwa, katika kukabiliana na changamoto ya Maafisa
Ustawi wa Jamii, kibali limetolewa cha kuajiri Maafisa hao 65 ambao
wamepangwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wakatekeleze sera
ya Mzee kwanza.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe Stanslaus
Nyongo amesema wabunge wapo tayari kuhakikisha mchakato wa kupitia sera
ya Wazee na kutungiwa sheria ya Wazee unakamilika.
Akizungumza
kwa niaba ya Wazee, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Mzee Lameck
Sendo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi kubwa anayoifanya ikiwemo
miradi mikubwa, kuhamasisha Utalii ambapo mingi imeongeza ajira kwa
vijana.
Amesema Wazee wapo pamoja na Mhe Rais. katika ujenzi wa Taifa ambapo
tangu
kuzinduliwa kwa baraza la Wazee ambao mchakato wake ulianza 1998 baada
ya utafiti kubainisha Wazee walikuwa na changamoto ya ukatili, kutengwa
na familia, kuachiwa mzigo wa Malezi ya watoto hawakuwa na pa kusemea.
"Jumla
ya mabaraza 20749 yameundwa tunaendelea kuimarisha Mawasiliano Kwa
mabaraza yote na kupata taarifa kwa muda mfupi" amesema Mzee Sendo.
No comments:
Post a Comment