NA MWANDISHI WETU, MBEYA
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI
imeahidi kuboresha miundombinu ya barabara na elimu kutokana na uwepo wa
changamoto hizo katika Jiji hilo.
Hayo
yamebainishwa leo Oktoba 5, 2022 na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Prof.
Riziki Shemdoe wakati akizungumza na Baraza la Madiwani wa Jiji hilo
mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua
miundombinu ya barabara shule za msingi na sekondari.
Prof.
Shemdoe amesema kuwa licha ya Mbeya kuwa Jiji bado lina changamoto
nyingi ambazo amejionea na kueleza kwamba Serikali ya awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kufanya
maboresho makubwa na ya kihistoria.
Akitolea
mifano ya hatua ambazo Serikali imeshakwisha anza kuifanya ndani ya
Jiji hilo, amesema kuwa hadi sasa tayari Halmashauri Jiji inaendelea na
utekelezaji wa miradi ya elimu yenye thamani ya zaidi ya Shilingi
Bilioni mbili.
Prof.
Shemdoe amesema katika kutelekeza hayo Serikali imepanga kutangaza
zabuni ya kuboresha barabara, kiwanja cha ndege na mifumo ya maji na
mwishoni mwa mwezi Oktoba na mwanzoni mwa mwezi Novemba 2022 na kazi
rasmi kuanza mwezi Machi 2023.
Baadhi
ya miradi aliyoitaja kuanza ni Pamoja na ujenzi wa stendi kuu ya mabasi
na stendi ndogo katika eneo la Airport ya zamani, Upanuzi wa barabara
ya Iziwa (km 5.75), Upanuzi wa barabara ya block T-Makunguru na Juhudi
(km 3.3), Upanuzi wa barabara ya uyole-Itezi (km 2.0), Upanuzi wa
barabara ya Airport-Samora-TANESCO-Sae-Kisanji na Kabwe Block T-Sido (km
3.2) Pamoja na uboreshaji na upanuzi wa mifumo ya maji eneo la Nzovwe.
Akishukuru
kwa niaba ya Baraza la Madiwani na wananchi wa Jijini Mbeya, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson ambaye ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo hilo, amesema
kuwa Jiji la Mbeya linayo Imani kubwa sana na Serikali ya Rais Samia na
kuiomba kuliangalia kwa jicho la upekee kutokana na kwamba Jiji hilo
limekuwa na hali mbaya katika sekta nyingi kwa muda mrefu.
“Ndugu
Katibu mkuu, changamoto zinazohusika na Ofisi yako zipo nyingi lakini
kwa hapa kwetu kipaumbele chetu kikubwa ni miundombinu ya barabara na
elimu, Kiukweli kabisa hali sio nzuri na uzuri wewe mwenyewe umetembelea
baadhi ya maeneo na umejionea hivyo basi tunakuomba ukitoka hapa
ulibebe hili kwa uzito mkubwa sana sana” amesisitiza Dkt. Tulia
Spika
wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
(Mb) akifurahi jambo na Katibu Mkuu-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe wakati
walipokuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya elimu na Barabara
Jijini Mbeya Oktoba 5, 2022 nyuma yake aliyekunja Mikono ni Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mhe. Triphonia Kisiga.
No comments:
Post a Comment