
WATUHUMIWA
40 wa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kuvunja nyumba
usiku maarufu panya road wamefikishwa mahakama ya Wilaya ya Ilala
Kinyerezi Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Jeshi
la Polisi, Dar es Salaam 6 Oktoba 2022 Mahakama ya Wilaya ya Ilala
Oktoba 5, 2022 imemsomea mashtaka Lubea Manzi maarufu Master, pamoja na
wenzake 39 waliofikishwa mbele ya Mahakimu watatu, Hakimu Mkazi Glory
Nkwera, Fadhili Luvinga, Rehema Liana, wakikabiliwa na mashtaka ya
unyang’anyi wa kutumia silaha na kuvunja nyumba usiku na kujeruhi watu
maeneo mbalimbali ya Wilaya, Ilala, Dar es Salaam.
Mwendesha
mashtaka wakili wa serikali Michael Momboko, Magdalena Kisoka, Aziza
Mhina walisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo tarehe 19
-21/09/ 2022 maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam ambapo
walivunja nyumba usiku na walipora mali baada ya kuwajeruhi wananchi kwa
kutumia silaha za jadi (mapanga, nondo, visu) na kukimbia.
Watuhumiwa
hao kwa pamoja walikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kutokana na
mashataka wanayowakabiliwa nayo kutokuwa na dhamana.
Kesi hiyo imeaharishwa mpaka tarehe 19/10/2022 na upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
No comments:
Post a Comment