NA MAKUBURI ALLY
TAASISI ya Michezo kwa Walemavu wa akili, Special Olympics Tanzania (SOT) imetoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo sambamba na serikali kuichangia timu ya Taifa inayotarajia kuiwakilisha nchi katika Soka, Riadha na Mpira wa Wavu kwenye michezo ya Dunia jijini Berlin mwakani.
Michezo ya Dunia kwa walemavu wa akili inatarajia kuanza Juni 12 hadi 26, 2023 jijini Berlin ambako Tanzania inatarajia kuwakilishwa na msafara wa wachezaji 22 na makocha zaidi ya nane watakaoambatana katika mashindano hayo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana Mkurugenzi wa SOT, Charles Rays alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau kuichangia timu hiyo inayohitaji zaidi Shilingi Bilioni 194 ambazo zitafanikisha maandalizi sambamba na ushiriki wa mashindano hayo makubwa.
Rays alisema hivi sasa ametuma barua katika taasisi mbalimbali ili ziichangie timu hiyo ambayo inahitaji uwezeshwaji utakaofanikisha kufanya vizuri katika mashindano hayo zikiwemo sare, tiketi na kambi ya maandalizi ya mashindano hayo.
“Nawaomba wadau wa michezo watusaidie kupatikana fedha hizo ambazo zitatuwezesha kushiriki kwa ufanisi michezo ya Dunia ambayo mara zote tunazoshiriki huwa tunarudi na idadi kubwa ya medali kwa sababu ya ubora wa wachezaji wetu,” alisema na kuongeza
Ofisini
kwetu, tuna idadi kubwa ya medali ya mashindano ya Dunia, hata msimu uliopita,
kwenye michezo iliyofanyika Abu Dhabi, Falme za Kirabu (UAE),” alisema Rays.
No comments:
Post a Comment