Ofisi
mpya za shamba la miti Mpepo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ambazo
zimewekwa jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa RuvumaKanali Laban Thomas
kwenye hafla ambayo imefanyika kwenye kijiji cha Mpepo.
SERIKALI
imetoa zaidi ya shilingi milioni 968 kujenga ofisi na nyumba tatu za
watumishi katika shamba la miti Mpepo linalohudumiwa na Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Akitoa
taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mhifadhi Mkuu wa
Shamba la Miti Mpepo John Kimolo amesema mradi wa ujenzi unatekelezwa na
Shirika la Nyumba NHC na kwamba jumla ya majengo manne yanajengwa
ikiwemo Ofisi kuu ya shamba,nyumba ya Mhifadhi na nyumba mbili za
watumishi.
Kimolo
amesema serikali inatekeleza mradi huo kwa lengo la kuboresha mazingira
bora ya kufanyia kazi na kuishi watumishi wa umma na kwamba mradi
umefikia zaidi ya asilimia 95 ya utekelezaji.
“Lengo
letu ni kuhamia Mpepo muda wowote,miundombinu ya mtandao wa intaneti na
umeme vitakapokamilika kwa sababu shughuli za kiofisi zinahitaji
mawasiliano ya mtandao’’,alisisitiza.
Hata
hivyo amezitaja changamoto zinazoikabili ofisi hiyo kuwa ni ubovu wa
barabara kutoka Nyoni hadi Mpepo inayopitika kwa shida hasa kipindi cha
masika,ukosefu wa umeme na moto wa mara kwa mara hasa kipindi cha
kiangazi unaosababishwa na wananchi wanapoandaa mashamba yao.
Akizungumza
mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali kupitia Rais Samia Suluhu
Hassan inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa
wa Ruvuma ukiwemo ujenzi wa ofisi za kisasa katika shamba la Mpepo.
Hata
hivyo Mkuu wa Mkoa amewaonya wananchi kuacha kuharibu mazingira kwa
kuchoma moto na kuharibu mazingira kwenye vyanzo vya maji ambavyo
amesema vinasababisha mabadiliko ya tabianchi.
Amewaagiza
viongozi katika ngazi zote kusimamia na kuunda Kamati za Mazingira
kwenye vijiji ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayechoma moto misitu na
amewataka wananchi kuacha tabia ya kuandaa mashamba kwa kuchoma moto.
“Sisi
ndiyo tunaochoma moto na kuharibu vyanzo vya maji,lakini sheria inasema
kwenye vyanzo vyote vya maji ndani ya mita 60 hakuna shughuli yeyote ya
kibinadamu inayotakiwa kufanyika,kuanzia sasa ni marufuku kulima au
kufanya shughuli zozote kwenye vyanzo vya maji’’,alisisitiza.
Shamba
la miti Mpepo ni miongoni mwa mashamba 24 ya miti yanayosimamiwa na
kuhudumiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara
ya Maliasili na Utalii.
No comments:
Post a Comment