SERIKALI
ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa
shilingi milioni 720 kuanzisha shule mpya mbili katika Halmashauri ya
wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
Mkurugenzi
wa Halmashari ya Wilaya ya Songea Neema Maghembe amezitaja shule hizo
kuwa ni shule ya sekondari Kizuka katika Kata ya Kizuka ambayo serikali
imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo.
Ameyataja
majengo ambayo yanajengwa katika sekondari hiyo kupitia fedha za
serikali za SEQUIP kuwa ni vyumba vinne vya madarasa,jengo la
utawala,maktaba, vyoo na jengo la TEHAMA.
Amesema
utekelezaji wa mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 95 na kwamba shule
inatarajia kuanza kuchukuwa wanafunzi kuanzia Januari 2023.
Mkurugenzi
huyo pia ameitaja shule tarajiwa ya msingi inayojengwa katika
kitongoji cha Lizaboni Kata ya Muhukuru iliyopo kilometa 140 kutoka
mjini Songea ambayo serikali imetoa shilingi milioni 250 kutekeleza
mradi huo.
“Mradi
huu unatekelezwa na fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi
milioni 250 ambazo zinajenga jengo la utawala,vyumba tisa vya madarasa
na samani zake na vyoo matundu 30’’,alisema Maghembe.
Hata
hivyo amesema mradi upo katika hatua za awali za utekelezaji na kwamba
mradi unatarajiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu ambapo Januari mwakani
shule inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi.
Akizungumza
baada ya kukagua miradi hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Stephen
Ndaki,ameipongeza Halmashauri hiyo kwa usimamizi unaofanywa kwenye
miradi,hata hivyo ameagiza kuwa na mpango kazi wa kutembelea na kukagua
miradi katika ngazi ya Halmashauri ili miradi iweze kutekelezwa kwa
ubora na kwa wakati.
Ameagiza
usimamizi unaofanywa kwenye miradi uheshimu kanuni za utawala
bora,uwazi na ushirikishwaji na kwamba Halmashauri zijitahidi kuzijengea
uwezo Kamati za Ujenzi ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija.
No comments:
Post a Comment