KUFANYIKA
kwa Mkutano wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Nchi mbali
mbali hapa Zanzibar kutasaidia kutangaza Fursa zilizopo pamoja na kukuza
Uchumi wake.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo
katika Hafla ya Chakula cha Usiku ilichoandaliwa na Taasisi inayosimamia
Makampuni yanayaondaa Misafara ya Watalii Zanzibar (ZATO) kwa Mabalozi
wa Tanzania Hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Park Hyyat Shangani Jijini
Zanzibar.
Mhe.
Hemed akiwakilishwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Simai
Mohamed Said ameeleza kuwa ni Fursa ya kipekee kwa Mabalozi hao
kutembelea Maeneo mbali mbali ya Zanzibar hatua ambayo itawasaidia
kuweza kuitangaza Zanzibar katika nyanja tofauti.
Ameeleza
kuwa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali
Mwinyi imeamua kujielekeza katika Dhana ya Uchumi wa Buluu kwa lengo la
kukuza Uchumi wake kwa kutumia Bahari.
Aidha
Mhe. Hemed amesema ana Imani Mabalozi hao wataitangaza Tanzania kwa
Mazuri yake na Fursa zilizopo ili Wawekezaji kuja kuwekeza na hatimae
Pato la Taifa liongezeke katika Pande zote mbili za Muungano.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameongeza kuwa Imani waliopewa Mabalozi hao
kuiwakilisha Tanzania ni muhimu kwao ambapo Taifa linawategemea katika
uwakilishi wao kwa Maslahi ya Wote pamoja na kuitangaza Tanzania Duniani
kote.
Sambamba
na hayo Mhe. Hemed ameipongeza Taasisi inayosimamia Makampuni
yanayaondaa Misafara ya Watalii Zanzibar (ZATO) kwa kuandaa Chakula
hicho na kuwataka Mabalozi hao kuwa karibu na Taasisi hiyo ikiwa ni
Taasisi muhimu katika kujenga Utalii endelevu kwa manufaa ya Tanzania.
Nae
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
Stergomena Lawrence Tax ameeleza kuwa kuwepo kwa Mkutano uliwakutanisha
Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Mataifa mbali mbali kumetoa
Fursa ya Mabalozi hao kufahamu mengi zaidi katika kuboresha utendaji wao
wa Kazi.
Aidha
Mhe. Tax ameipongeza ZATO kwa kuandaa Chakula hicho cha Usiku na
kueleza kufarishwa na maamuzi hayo na kuahidi kuendelea kuwa karibu nao
ili kukuza Sekta ya Utalii Tanzania.
Mapema
Mwenyekiti wa Taasisi inayosimamia Makampuni yanayaondaa Misafara ya
Watalii Zanzibar Ndugu Hassan Ali Mzee ameeleza kuwa Mabalozi hao ni
sehemu ya kutangaza Utalii wa Tanzania ambapo uwepo wao katika Nchi
wanazofanya kazi itasaidia kurahisisha huduma bora kwa Watalii wanaokuja
Nchini Tanzania.
Ameeleza
kuwa bado Zanzibar inakumbwa na wasambaza watalii wasio rasmi na
kuwataka Mabalozi hao kuhamasisha Watalii wanaokuja Zanzibar kutumia
Makampuni yaliyosajiliwa kisheria ili kupata Huduma bora kipindi chote
wanapokuwa Zanzibar.
Waziri
wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Simai Mohaemd Said akizungumza katika
Hafla ya Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Taasisi inayosimamia
Makampuni yanayoandaa Misafara ya Watalii Zanzibar (ZATO) kwa Mabalozi
wa Tanzania akimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed
Suleiman Abdulla iliyofanyika Hotel ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stegomena
Lawrence Tax akizungumza na mabalozi na wageni mbali mbali waliohudhuria
katika hafla ya chakula cha usiku kwa mabalozi wa Tanzania iliyofanyika
hotel ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment