Tanzania
inashiriki katika Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika la
Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kujadili taarifa mbalimbali za
utendaji kazi wa ARIPO na kupitia taarifa mbalimbali za Itifaki
zinazosimamiwa na ARIPO
Mkutano huo ulioanza, Jana
Novemba 21, 2022 Maputo, Msumbiji, unahudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa,
Afisa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar
(BPRA), Bi. Mariam Jecha Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu Bw. Seka
Kasera pamoja na mwakilishi kutoka ofisi ya Hakimiliki Tanzania Bw.
Philimon Kilaka.
BRELA kama Ofisi ya MIliki Ubunifu nchini
imekuwa mshiriki mkubwa wa ARIPO kwenye masuala mbalimbali yanayohusu
Miliki Ubunifu kwenye Ukanda wa Afrika. Katika Mkutano huo masuala
mbalimbali yatajadiliwa hasa kuhusu Hataza, Maumbo Bunifu, Alama za
Biashara na Huduma, Hakimiliki na linzi zingine za Miliki Ubunifu.
Wadau
mbalimbali wa ARIPO ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Kimataifa na
Kikanda wameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano. Kwa upande wa Shirika la
Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) limewakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO
Bw. Daren Tang.
Mkutano huo wa siku tano utakaohitimishwa tarehe
25 Novemba, 2022 umefunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa
Msumbiji, Mhe. Silvino Mareno.
Nchi wanachama 22 wa ARIPO zinashiriki ikiwa ni pamoja na WIPO na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa.Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.
Godfrey Nyaisa(wa pili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), Bi. Mariam Jecha(kulia),
wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkugenzi wa Miliki Ubunifu
(BRELA) Bw. Seka Kasera (kushoto) na Mwakilishi wa ofisi ya Hakimiliki
Tanzania Bw. Philemon Kilaka ( wa pili kulia) mara baada ya ufunguzi wa
Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika Miliki Bunifu kanda ya
Afrika(ARIPO) unaofanyika kwa siku tano Maputo, Msumbiji.
Washiriki
wa Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Miliki Ubunifu
Kanda ya Afrika (ARIPO), wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya
ufunguzi wa mkutano huo mapema leo tarehe 21 Novemba, 2022 Maputo,
Msumbiji
Monday, November 21, 2022
New
BRELA YAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA MKUTANO MKUU WA 46 WA ARIPO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment