Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imewatoa hofu watumiaji wa usafiri wa Anga nchini kuhusu usalama katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba uliopo katika Manispaa ya Mji Bukoba Mkoani Kagera baada ya kutokea kwa ajali ya Ndege ya Precision Air ATR 42-500 yenye namba PW 494 iliyoanguka kwenye ziwa Victoria mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikijiandaa kutua siku ya Jumapili Novemba 06, 2022.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari amewaomba watanzania na hasa
watumiaji wa Usafiri wa Anga kuwa watulivu kwa kuwa uwanja wa ndege wa
Bukoba ni salama kwa matumizi ya Usafiri wa Anga na kuomba wanaotoa
taarifa potofu kuwaachia wataalamu wa uchunguzi wa ajali za ndege
kuendelea na uchunguzi wa ajali iliyotokea.
Amesema
kwenye Sekta ya Usafiri wa Anga ajali hii sasa ni sehemu ya kujifunza,
ili kupitia kwa haya yaliyotokea na kujiwekea mikakati jambo la namna
hii lisiweze kutokea tena katika usafiri wa anga huko mbeleni kwani
usafiri wa anga ndio usafiri salama Duniani.
Pia
amesema kitaalam inapotokea viwanja vya ndege upande mwingine kuwa
karibu na maji, viwanja vya namna hiyo vina faida kwasababu kwenye maji
kuna vikwazo vichache sana na hata ndege ikianguka kwenye maji madhara
yake yanakuwa madogo ukilinganisha na nchi kavu ambapo zinaweza
kupelekea moto.
Amesema
uwanja wa ndege wa Bukoba una urefu wa kilometa 1.5 na uwanja huo
unauwezo wa kuhudumia ndege zenye uzito mpaka wa tani 29. Na kuongeza
kuwa ndege ya Precision Air ATR 42-500 yenye namba PW 494 iliyopata
ajali ilikuwa na uzito wa tani 18.5.
Mkurugenzi
Johari ameongeza kuwa ndege hiyo kwa aina yake ili iweze kutua
inahitaji urefu wa mita 900 na wakati wa kupaa inahitaji urefu wa
kilometa 1.1, hivyo kutakana na vigezo hivyo uwanja wa ndege wa Bukoba
unakidhi vigezo hivyo .
Ametoa
angalizo kwamba, kusambaza taarifa mbalimbali za ajali bila utaratibu
uliowekwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani ni kosa na
tunaweza kuiweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoridhia na kusaini
mkataba wa Chicago katika maangaiko yasiyokuwa ya msingi, hivyo ni
vizuri kutulia na kuwaacha wataalamu wakafanya kazi yao vizuri na bila
kuingiliwa.
Ametoa
mfano kwamba , jana kuna mtu katengeneza video yake ya uongo ikionesha
ndege ilivyokuwa inakwenda pale mpaka inadondoka ndani ya maji na
ameweka nembo ya Shirika la Ndege la Precision Air, kufanya hivyo ni
kosa kwa mujibu wa sheria na hali hii imeongeza taharuki kwa watumiaji
wa usafiri wa anga pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kuamini kuwa kile
kilichotengenezwa kimetolewa na mamlaka husika na wengine wanajiuliza
hii imetoka kwenye rada za TCAA.
Mkurugenzi
Hamza ameongeza kuwa Jumuiya za huko nje zinashangaa kuna kitu gani
kimetusibu maana bado tuna msiba huku baadhi ya watu hawatulii nchi hii
wakawaacha wataalam wakafanya kazi zao kitaalam na kuja na majibu mazuri
ili kuutangazia umma kuhusu sababu kubwa iliyopelekea ndege kudondoka
kwenye maji.
Ametoa
shukrani kwa wadau wote wakiwemo wavuvi, Sekta Binafsi, Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege(TAA) kwa kuweza kusimama kidete kuhakikisha watu kwenye ndege
wanatoka salama.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari
akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa Uwanja wa
Ndege wa Bukoba baada ya kutokea kwa ajali ya ajali ya Ndege ya
Precision Air ATR 42-500 yenye namba PW 494 iliyoanguka kwenye ziwa
Victoria mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikijiandaa kutua
siku ya Jumapili Novemba 06, 2022.
Baadhi
ya maofisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)
wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza S.Johari
alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa
Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Rubani
wa Ndege Kapteni Noel Komba akizungumza kuhusu uwanja uwanja wa ndege
wa Bukoba wakati wa mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari alipokuwa anazungumza na waaandishi
wa habari kuhusu hali ya usalama wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba baada ya
kutokea kwa ajali ya ajali ya Ndege ya Precision Air ATR 42-500 yenye
namba PW 494.
No comments:
Post a Comment