Na. Hassan Kimweri - WAF, Morogoro
Wizara
ya Afya kwa kutambua mchango wa jamii na viongozi wao katika kuongeza
kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO-19, Jana ilizindua rasmi awamu ya pili
ya kampeni hiyo Mkoani Morogoro.

"Sisi
kama Serikali tumeruhusu wananchi wetu wachanje kwa hiyari kwa kuwa
chanjo hii haina madhara yoyote katika mwili wa binadamu na mimi
nimechanja na niko salama." Amesema Mhe. Msando
Mhe.
Msando amewatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kubweteka kwakuwa
wengine hawasikii habari za UVIKO-19 lakini ugonjwa huo upo tuendelee
kuchukua tahadhari, pia tujitokeze kupata chanjo ya ugonjwa huo ili wote
tuendelee kuwa salama.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga-Wizara ya Afya Dkt. Beatrice
Mutayoba amesema kila chanjo zinapoingia nchini zinapimwa ili
kujiridhisha na usalama wake kwakuwa chanjo hizo zinakwenda kutumika kwa
watanzania.
"Hata
tukikumbuka wakati wa uzinduzi wa awamu ya kwanza kwa utoaji wa chanjo
ya UVIKO-19 Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan alikuwa wa kwanza kupata chanjo hiyo hivyo chanjo hii ni salama."
Amesema Dkt. Mutayoba
Naye,
Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amewashukuru wananchi wa
Mkoa wa Morogoro kwa kujitokeza kupata huduma hiyo ya chanjo kwakuwa
tayari wamepata elimu na kujua chanjo hiyo ni Salama.
"Mimi
nimechanja tarehe 24 Julai, 2021 na hadi sasa niko vizuri na hata
nyumbani pia niko vizuri, chanjo hii haina madhara yeyote ni kama chanjo
nyingine kwa kuwa lengo lake ni kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19."
Amesema Bw. Msigwa
Mwisho,
Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Morogoro Bw. Masumbuko Ijembya
amesema Mkoa huo ulianza rasmi kutoa chanjo ya UVIKO-19 Agosti 3, 2021
hadi kufikia Octoba 31, 2022 wamefikia asilimia 66.2 ya utoaji wa chanjo
hiyo kwa wenye umri zaidi ya miaka 18.
"Leo
(jana) hii tumefanya uzinduzi huu mkoani hapa kwa lengo la kuongeza kasi ya
uchanjaji kwa kufikia zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wote wenye umri
zaidi ya miaka 18 wawe wamepata chanjo ya UVIKO-19." Amesema Bw.
Masumbuko
Kampeni
hii itaendelea katika mikoa saba mingine ambayo ni Pwani, Katavi,
Rukwa, Manyara, Tanga, Simiyu na Singida na katika kila mkoa kampeni
itaendeshwa katika kila halmashauri na kata zote ndani ya halmashauri
husika, Lengo likiwa ni kusogeza zaidi huduma hii mahali alipo kila
mwananchi.
"Bega kwa Bega, Ujanja Kuchanja"
No comments:
Post a Comment