Na John Walter-Babati
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara kimefanya tafrija
ya kumuaga aliyekuwa Katibu wa chama hicho Daniel Muhina baada ya
kuhamishwa kikazi kutoka mkoani hapa kwenda mkoani Kagera.
Wanachama
hao Wilaya ya Babati, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wamemuaga
Katibu huyo wa Babati Mjini Daniel Muhina aliyehamishiwa wilayani
Bukoba Mjini Mkoa wa Kagera kwa majukumu kama hayo ndani ya Chama,
hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kisora Usiku wa kuamkia leo Desemba
11,2022.
Wanachama hao wamemtakia kila la kheri Muhina huko aendako, wakimshukuru Kwa utekelezaji wake uliotukuka.
Muhina
amesema amefanya kazi ya kuwatetea waliokuwa na Mazingira magumu ndani
ya Chama jambo ambalo halikuwapendeza wengine, ikiwa ni pamoja na
kufanikisha ajira ya kudumu kwa sekretari wa Chama aliyekuwa akijitolea
kwa muda pamoja na kutengeneza Mazingira mazuri ya kuanzia ujenzi wa
nyumba ya dereva wa Chama.
Muhina anaeleza alipoona Mazingira ya
uonevu ndani ya chama alisimama mstari wa mbele kuwatetea huku wengine
bila kuwataja majina yao wakimpinga.
Amewaachia ujumbe wanachama wa CCM kupendana huku akiwakumbusha kuwa kuna leo na kesho.
Akizungumza
kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mati super Brand Ltd, meneja ugavi na
ununuzi Aikande Lema, amesema kipindi chote walishirikiana kwa karibu na
katibu huyo kufanikisha masuala mbalimbali.
Mbunge wa zamani wa
jimbo la Babati Vijijini na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa
Vrajlal Jitusoni amesema kazi ya chama hicho ni Kubwa kwa Wananchi na
kina uhakika wa kuchukua Dola mwaka 2025.
Muhina amehudumu kama
Katibu mkuu CCM Manyara tangu mwaka 2021 Hadi mwaka 2022 akikisimamia
Chama hicho na serikali kutekeleza ilani iliyopo.
Amehamia katika
Mji wa Bukoba ambapo hapakuwa na katibu kwa miezi miwili huku Babati
Mjini pakiwa wazi kwa zaidi ya miezi miwili na hakuna alietangazwa
kuziba nafasi hiyo.
Hata hivyo tukio hilo pia limehudhuriwa na
Katibu Tawala Wilaya ya Babati Khalfan Mathipula ambaye amesema Muhina
alikuwa ni daraja zuri kati ya chama na Serikali.
No comments:
Post a Comment