AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TEMBO MKOANI LINDI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, August 13, 2023

AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TEMBO MKOANI LINDI


MTU mmoja anayefahamika kwa jina la Saidi Kuleni (40-45) mkazi wa Likwela, Nachingwea - mkoani Lindi, amefariki baada ya kukanyagwa na Tembo akiwa shambani.

Shuhuda wa tukio hilo Mustapha Abdallah amesema alifanikiwa kumwona marehemu baada ya kuwa na mashaka na eneo la tukio ambalo lilikuwa na alama nyingi za miguu ya Tembo pamoja na baiskeli.

Mustapha amesema, siku ya Agosti 11, 2023 akiwa anaelekea shambani majira ya saa kumi alasiri katika kijiji cha Narungombe, aliiona baiskeli imeegeshwa porini na wakati huo hakuwa na shaka hadi alipoikuta tena baiskeli ile siku ya tatu baadaye majira ya asubuhi (Agosti 13, 2023).

Viongozi wa kijiji hicho pamoja na shuhuda ambao wote ni wakulima wamesema hali ya usalama kijijini hapo na shambani ni tete kwasababu ya kuvamiwa na shehena kubwa ya Tembo ambao wamekuwa chanzo cha wananchi kutoishi kwa raha na kuhofia usalama wao.


SOURCE - EastAfricaTV

No comments:

Post a Comment