IMEBAINISHWA kuwa
asilimia 94 ya majeruhi wa mifupa na ubongo hupokelewa katika Taasisi ya Tiba
ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) masaa sita baada ya kutokea kwa ajali
kinyume na viwango vya kimataifa vinavyotaka majeruhi kufikishwa hospitalini
hapo ndani ya saa moja ili kuokoa maisha yao.
Hayo yamebainishwa
leo katika kikao cha kimkakati baina ya MOI na hospitali ya za Mkoa wa
Dar es Salaam na Pwani kwa lengo la kuboresha huduma kwa majeruhi wa mifupa
,mgongo na ubongo.
Katika kikao hicho
kilichofanyika MOI kwa lengo la kuboresha matumizi ya ‘saa la dhahabu’
inayomtaka majeruhi kupata matibabu ya uhakika ndani ya saa moja tangu kutokea
kwa ajali.
Mkuu wa kitengo cha
utafiti MOi Dkt.Joel Bwemelo amesema kuchelewa kufikishwa majeruhi
hospitalini hapo kunapunguza uwezekazo wa kunusuru maisha yao.
“Kuna saa moja la
dhahabu linaloweza kuokoa msiaha ya majeruhi tangu ajali itokee…hapa MOI
asilimia 94 ya majeruhi huja masaa sita tangu kutokea kwa ajali, wakati huu ule
muda wa saa la dhahabu la kuokoa maisha yake huwa limepita”
Kwa upande wake
Dkt. Anthony Assey amesema miongoni mwa sababu za kucheleweshwa kwa majeruhi
kufika MOI ni pamoja na utaratibu wa rufaa unachokua muda mwingi na kwamba
kikao hicho kinalenga kuboresha mfumo wa rufaa ili kuwawahisha wangonjwa
kufika.
“Kitu cha msingi
kabla ya kumrufani majeruhi, hakikisha umemuhidumia na amekuwa stahimilivu
(stabilize), tukumbuke kuna suala la barabara zetu, foleni, hivi vyote
vinahitaji kuzingatiwa kwa kumuandaa majeruhi kuweza kuhimili hali hiyo ili
asipate athari za pili” amesema Dkt. Assey
Naye mratibu wa
kikao kazi hicho Dkt. Bryson Mcharo amesema lengo ni kuondoa changamoto
zinazozuia majeruhi kupatiwa matibabu ndani ya saa moja tangu kutokea kwa
ajali.
Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana Dkt. Bryson Kiwelu ameipongeza MOI
chuni ya utaratibu mpya utakaowawezesha kumpa rufaa majeruhi kwenda MOI moja
kwa moja bila ya kupitia hospitali zingine.
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt. Laurent Lemery amesema kikao hicho kinalenga kutetekeleza
sera ya wizara ya afya ya kuboresha utoaji huduma na hasa kwa wagonjwa
wanaopata rufaa kwa ajili ya kuja MOI kwa matibabu zaidi.





No comments:
Post a Comment