NA MWANDISHI WETU, DODOMA
SERIKALI imetoa jumla ya shilingi trillioni 1.7 kwa Wakala
wa Nishati Vijiini (REA)kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
nishati nchini.
Aidha
Serikali imetoa billion 12 kwa ajili ya mradi wa kuwezesha ujenzi wa vituo
Vidogo vya kusambaza bidhaa za Petroli na Diseli vijijini Tanzania bara kwa
lengo la Kulinda Mazingira na Afya ya Watumiaji na Kuboresha upatikanaji na
Usambazaji wa Mafuta vijijini.
Mkurugenzi
Mkuu Wa Wakala wa Nishati Vijiini REA Mhandisi Hassan Said amesema hayo leo
Jijini Dodoma katika Mkutano na waandishi wa Habari akisema usambazaji wa mradi
huo unahusu kuwekeza ujenzi wa vituo Vidogo vya mafuta Katika maeneo
mbalimbali Vijiini.
"Tumeandaa
programu maalumu ya kuhamasisha matumizi bora ya nishati na hii ni kuwaelimisha
kina mama kwamba unaweza kitumia umeme kuzalisha mali ambapo upatikanaji wa
umeme maeneo ya vijijini asilimia 69.6% vijiji 10600 vimefanikiwa kufikiwa
tunamaliza kupeleka umeme kwenye vijiji sasa tunaanza kwenye
vitongoji"Amesema Mhandisi Saidi.
Moja
ya changamoto inayosababisha wananchi wasitumie nishati safi na kuendelea
kutumia nishati ya asili yaani Mkaa na Kuni ni Pamoja na upatikanaji wake kwani
nishati asilia zimekua zikipatikana kwa urahisi.
Mhandisi
huyo amesema Wakala umeanza kutekeleza Mradi wa kusambaza mitungi ya gesi ya
kupikia kwa utaratibu wa utoaji ruzuku kuwezesha usambazaji wa mitungi ya gesi
ya kupikia (LPG) 71,000 yenye thamani ya shilingi bilioni 3 pamoja na
majiko banifu 200,000 (laki mbili) katika maeneo ya vijijini huku Kwa
Mwaka wa Fedha 2023/24 Jumla ya fedha takribani bilioni 10 zimetengwa
kwaajili ya kufanikisha mradi huo.
"Tumefanikiwa
kuja na programu ya kuwezesha majiko banifu na serikali imepata udhamini kutoka
benki ya dunia kwa shilingi bilioni 14 pamoja na programu ya kuwezesha
uzalishaji mkaa mbadala ili utumike badala ya kuni na mkaa"
Ametoa
Rai kwa Watanzania kutumia mafundi wanaotambulika na Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kuondoa lawama zinazotolewa na wananchi dhidi ya Serikali
zinazosababishwa na mafundi vishoka wanaotumia njia za magendo kufanya shughuli
hizo za uunganishaji wa Umeme.
"Tumedhamiria
kuanzisha usambazaji wa mitungi ya gesi kila mkoa 2,700 na hii mitungi mtu
anaweza kuiona ni midogo lakini tumekusudia kuhamasisha wananchi kutumia gesi
na kuhamasisha wananchi kutoka kutumia mkaa na kuni ikiwa ni ajenda ya kutunza
mazingira na kutoka kwenye nishati chafu hadi nishati safi" Amesisitiza
Mhandisi Saidi
Kadhalika
Serikali kupitia REA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) imetenga Dola za
Kimarekani (USD Milioni 6) kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa majiko banifu ya
kupikia.
Kabla
ya Wakala wa Nishati Vijiini kuanzishwa nchini upatikanaji wa Umeme Vijiini
uliku chini ya asilimia 5% na kufikia asilimia 69.6 za sasa.
Aidha
wakala wa Nishati Vijijini(REA)imedhamiria kuboresha maisha ya wananchi waishio
vijijini kupitia upatikaji wa Nishati.






No comments:
Post a Comment