NA MWANDISHI WETU, SAME
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Nurdin Babu ametoa wiki mbili kwa Kamati ya Ujenzi ya Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) maabara na nyumba ya mtumishi katika zahanati ya Naibili wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kuhakikisha unakamilika.
Babu ameyasema hayo akiwa
kwenye ziara wilayani humo kukagua miradi mbalimbali
ya maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali
ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
"Dk Samia ametoa zaidi ya shilingi milioni 271, lengo ni wananchi
wake wapate huduma za afya kwa wakati, sipo tayari kuona ujenzi huu unasuasua,
hivyo naagiza kituo hicho kijegwe usiku na mchana," amesema Babu.
Mkuu huyo wa mkoa, amewataka kila kiongozi kwa
nafasi yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha kujua kila mradi unaotekelezwa
katika sekta yake kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha unamalizika ukiwa na
viwango vya hali ya juu.
Would by far have the choice to make on faint spot interests! Welcome to here you'll find how it should look. Wikipedia account registration guide
ReplyDelete