NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya
Siasa Nchini, utakaokutanisha wadau wa siasa lengo likiwa kuthamini utekelezaji
wa mapendekezo ya kikosi kazi utakaofanyika Agosti 28 mwaka huu jijini Dar
es salaam.
Akizungumza leo Agosti 21 jijini Dar es Salaam,
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi, amesema mkutano huo
unaotarajia kufanyika Agosti 28, utawakutanisha wadau wa siasa mbalimbali ambao
utafanyika Kwa siku tatu katika kituo cha Mikutano ya Kimataifa Julius Nyerere
(JNICC).
Amesema kuwa lengo la mkutano huo maalum ni
kujadili hali ya siasa nchini na tathimini ya utekelezaji wa ushauri wa kikosi
kazi uliotolewa kwa Serikali .
“Mkutano huu tunatarajia
utafunguliwa na Rais Dk.Samia na unatarajia kufungwa Agosti 30 mwaka huu na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ,”
amesema Jaji Mutungi.





No comments:
Post a Comment