KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YATEMBELEA KITUO CHA MAARIFA WILAYA YA MANYONI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 10, 2023

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YATEMBELEA KITUO CHA MAARIFA WILAYA YA MANYONI

 

 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga akizungumza na wananchi na wakazi wa halimashauri ya Manyoni wanaopata huduma katika kituo cha maarifa Manyoni mara baada ya kutembelea kituo hicho alipokuwa ameambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI October 10,2023 kwa lengo la kutembelea shughuli zinazotekelezwa na TACAIDS.

..................................................

NA NADHIFA OMAR , MANYONI 

KITUO cha Maarifa cha Manyoni kimechangia katika mikakati ya taifa ya Mkoa wa Singida ya utoaji elimu ya kupunguza ongezeko la maambukizi ya VVU, kutokanana kujengwa kando kando ya barabara yanapoegeshwa magari ya masafa marefu ikiwa ni hatua ya inayoelenga kufikia makundi yaliyo katika uhatarishi wa kupata maambukizi ya mapya ya VVU.

Hayo yamejiri leo tarehe 10Octoba,2023 wakati Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI ilipotembelea kituo cha Maarifa cha Manyoni na Kujionea shughuli zinazotekelezwa katika kituo hicho.

Akiwasilisha taarifa ya kituo hicho mganga Mkuu wa Halimashauri ya Manyoni DktFuraha Mwakafwila amesema kuwa kituo hicho kilijengwa na TACAIDS kwakushirikiana na Mgodi wa Geita Gold Mining ikiwa ni moja ya jitihada za serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kupambana na maambukizi mapya ya VVU.

‘Kituo hiki kilijengwa mwaka 2016 na TACAIDS kwa kushirikiana na GGM ambapo kiligharimu jumla ya Shilingi za kitanzania 87,584,077. Lengo ikiwa ni ni kutoa huduma kwa madereva wa masafa marefu,wasafiri wanaotumia barabara kuu Dar es Salaam,Tabora na Singida pamoja na watu wote wanaoishi manyoni”amesema Dkt Furaha Mwakafwila.

Aidha ametoa taarifa ya huduma ya upimaji wa VVU katika kituo hicho kuanzia mwaka 2022 hadi 2023 jumla ya watu 1990 wamepima afya zao,ambapo wanaume ni 983 na wanawake ni 1007,madereva ni 684.jumla ya watu 19 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU ikiwa ni pamoja na kuunganishwa katika kliniki za Tiba na Matunzo.

Ameipongeza serikali kwa wazo la kushirikisha wadau na kuona umuhimu wa kujenga kutuo hicho katika halimashauri ya Manyoni ili upimaji wa VVU,Condomu pamoja na kupata ARV kwa wale ambao tayari wamepima kuanza dawa waweze kuchukua dawa iwapo itatokea mtu kaishiwa akiwa safarini,hasa kwa madereva wa masafa marefu,wasafiri wanaotumia barabara kuu Dar es Salaam,Tabora na Singida pamoja na watu wote wanaoishi Manyoni.

Ameongeza kuwa anashukuru kituo hiki kuongezewa huduma za zahanati kwani zimepelekea kituo hiki kuimarika zaidi na kuendelea kukuwa kwani sasa wananchi wanaozunguka katika eneo hilo ndio imekuwa zahanati yao kuu ya kupata huduma zote,kwakuwa awali ilikuwa ni kwa ajili ya huduma za HIV tu tofauti na sasa.

Dkt Mwakafwila amewataka wakazi wa manyoni kuja kituoni hapo kupata huduma zote za afya zipo na watoa huduma wapo,wananchi wasihangaike kwenda mbali kwa ajili ya kutafuta huduma za Afya.

Alibainisha baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa kituoni hapo kuwa ni pamoja na kituo kusajiliwa kutoa kutoa huduma za NHIF na CHIF,kuongezeka kwa idadi ya wateja hasa akina mama katika kliniki ya huduma za mama na mtoto.

Pia kuongezeka kwa wateja wanaokuja kupata huduma za ushauri nasaha na kupima afya zao ,kupata kisima chenye maji mengi ambayo yamekuwa msaada kwa kituo hicho pamoja na wakazi wa jirani, kiuto kusajiliwa kutoa huduma ya Tiba na matunzo (CTC).kuwepo kwa kamati ya maborshao na matunzo pamoja na kuundwa kwa vikundi vya utoaji Elimu kwa jamii.

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga mewapongeza watendaji wa kituo hicho kwa kazi nzuri wanaoitaka na kuwataka wananchi wa halmashauri ya Manyoni kuto sita kutembelea kituo hicho ili kupata huduma zinazotolewa.

Pamoja na ziara hiyo baadhi ya wabunge walishiriki kupima VVU na kendelea kuhamasisha umma, wa kila mmoja kujua afya yake.


Dkt Ainea Mlewa Mratibu wa UKIMWI –Afya halimashauri ya Wilaya ya Manyoni akifafanua namna wanavyotekeleza majukumu yao kituoni hapo wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI, wanaomsikiliza ni baadhi ya wabunge wa kamati hiyo, na aliyekaa amevaa sare nyeupe ni Muhudumu wa Afya Kituo cha Maarifa Manyoni Bi Getrude Sebastian.

Mhe Cecil Mwambe mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI akipata huduma ya kupima VVU katika kituo cha Manyoni mara baada ya kutembelea kituo hicho na kuelezwa huduma zinazotolewa katika kituoni hapo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI(Kamati haonekani katika picha)  kuhusu chimbuko la ujenzi wa vituo vya maarifa walipokuwa katika kituo cha maarifa Manyoni wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kutembelea shughuli zinazotekelezwa na TACAIDS kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga. 

 Mhe Hassan Haji Kassim Mjumbe Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI akipata huduma ya upima wa VVU wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI katika kituo cha Manyoni Mkoani Dodoma tarehe 10 Octoba,2023.

No comments:

Post a Comment